![Mzawa Blog Tz Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1748557994516725760/spgyJF7V_x96.jpg)
Mzawa Blog Tz
@mzawablog
Followers
103K
Following
229K
Statuses
155K
| Ukurasa rasmi wa X wa Mzawa Online | The Official X account of Mzawa Online | #NewsWithUs🌍 | #SisiNaHabari | Time: 24hrs🎙️
Dar es Salaam, Tanzania
Joined July 2015
VIDEO: Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Dkt. Selemani Jafo, ameiagiza TanTrade kuhakikisha kwamba ndani ya miezi mitatu, mchakato wa kupata chapa ya "Made in Tanzania" uwe umekamilika ili iweze kuzinduliwa rasmi katika maadhimisho ya Sikukuu ya Sabasaba. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na nembo yake rasmi kwa bidhaa zake ili kuzitangaza katika masoko ya kitaifa na kimataifa, kuongeza ushindani na kusaidia katika ukusanyaji wa takwimu za kibiashara. Dkt. Jafo ameyasema hayo wakati wa hafla ya kutangaza bunifu zilizoshinda chapa hiyo, iliyofanyika Februari 11, 2025, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Mh. Sempeho Manongi, Mkurugenzi wa TanTrade, Bi. Latifa Khamis, pamoja na viongozi wengine.
0
0
0
VIDEO: Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Dkt. Selemani Jafo, ameiagiza TanTrade kuhakikisha kwamba ndani ya miezi mitatu, mchakato wa kupata chapa ya "Made in Tanzania" uwe umekamilika ili iweze kuzinduliwa rasmi katika maadhimisho ya Sikukuu ya Sabasaba. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na nembo yake rasmi kwa bidhaa zake ili kuzitangaza katika masoko ya kitaifa na kimataifa, kuongeza ushindani na kusaidia katika ukusanyaji wa takwimu za kibiashara. Dkt. Jafo ameyasema hayo wakati wa hafla ya kutangaza bunifu zilizoshinda chapa hiyo, iliyofanyika Februari 11, 2025, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Mh. Sempeho Manongi, Mkurugenzi wa TanTrade, Bi. Latifa Khamis, pamoja na viongozi wengine.
0
0
1
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Sempeho Manongi, amesema kuwa lengo la kuwa na chapa hii ni kutambulisha bidhaa zote zinazotengenezwa Tanzania ili zijulikane ndani na nje ya nchi. Aidha, amesema kuwa Dunia inapaswa kutambua kwamba Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa zenye ubora. Ameyasema hayo katika hafla ya kutangaza chapa tatu bora zilizoshinda kati ya 80 za Made in Tanzania, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) mnamo Februari 11, 2025.
0
0
0
Klabu ya Young Africans SC (Yanga SC) leo, tarehe 11 Februari 2025, imesherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1935. Yanga SC, timu kongwe na yenye mafanikio zaidi nchini Tanzania, imetimiza miaka 90 tangu kuanzishwa kwake, huku kipindi chote hicho kikishuhudia nyakati tofauti za kisoka, changamoto za kiuchumi, pamoja na kupanda na kushuka kwa matokeo uwanjani. Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa mataji mengi, ikiwemo: Mataji 30 ya Ligi Kuu Tanzania Bara Mataji 3 ya Kombe la Nyerere Mataji 4 ya Kombe la FAT Mataji 7 ya Kombe la Tusker Mataji 3 ya Kombe la Mapinduzi Mataji 8 ya Ngao ya Jamii Mataji 5 ya Kombe la CECAFA @Yanga1935
0
0
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Uwekezaji wa Kituo cha Kisasa cha Ukaguzi na Upasishaji wa Vyombo vya Moto ni Mapinduzi Makubwa katika Sekta ya Usafiri hapa Nchini . Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza katika Ufunguzi wa kituo hicho Kwasilva kiliopo Dole Kizimbani Wilaya ya Magharibi A ,Mkoa wa Mjini Magharibi . Kituo hicho ambacho ni Ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Kizalendo ya Zenj General Mechandize kina Uwezo wa kuhudumia Vyombo vya moto Takribani 300 kwa Siku kwa kutumia mashine na Teknolojia ya Ukaguzi yenye Viwango vya Kimataifa. Aidha Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kituo hicho ni muhimu kwa Ukuaji na Maendeleo ya Sekta ya Usafiri na kitafungua Ukurasa Mpya wa Usalama wa Usafiri Barabarani. Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuthamini na kushirikiana na Sekta binafsi kufanikisha miradi ya Uwekezaji ya ndani na ile inayotoka nje ya nchi kwa mafanikio makubwa. Akizungumzia Usafiri wa Umma Dkt.Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuwa na Usafiri wa Mabasi ya Kisasa ya Umeme yatakayotoa huduma Bora kwa Wananchi . Akiwasilisha Taarifa ya Kitaalamu ya Mradi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi Habiba Hassan amesema Mradi huo wa Ubia baina ya Kampuni ya Zenj General Mechandise na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umegharimu Shillingi Bilioni 2.8 hadi kukamilika kwake na una Uwezo wa kukagua Vyombo vya Moto 300 kwa siku. @ikuluzanzibar
0
0
2
Mkurugenzi wa TANTRADE, Bi. Latifa Khamis, amesema kuwa ni muhimu kuwa na chapa ya "Made in Tanzania" kwa lengo la kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinapata haki ya ubora. Nembo hiyo itatambulisha bidhaa zetu katika masoko ya ndani na nje ya nchi, ili Tanzania ijivunie chapa yake. Bi. Latifa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya kutangaza bunifu bora tatu zilizoshinda chapa hiyo. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere International Conference Center (JNICC) tarehe 11 Februari 2025, na imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Mh. Sempeho Manongi, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hashil Abdallah, pamoja na Mkurugenzi wa TANTRADE na viongozi mbalimbali.
0
1
2
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dkt. Selemani Jafo, ametoa wito kwa watumishi wa taasisi zote nchini kuhakikisha wanajenga mazingira ya kuheshimiana na kuthaminiana. Amezungumza hayo wakati wa uzinduzi rasmi bodi ya uongozi ya chuo cha elimu ya Biashara CBE 10 Februari 2025, Waziri Jafo amesisitiza umuhimu wa watumishi kuwa na sifa ya kuthamini juhudi na vipawa vya wenzao ili kuongeza tija katika sekta mbalimbali za maendeleo.@ViwandaBiashara @cbeofficial1965
0
1
0
VID3O: Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Dkt. Selemani Jafo, amewahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali itafanyia kazi malalamiko yao kuhusu tozo ya kupandisha na kushusha makontena. Vikevile Waziri Jafo amesema ndani ya siku 60 Serikali itaitisha Mkutano mwingine baada ya kukaa na sekta husika ili kupata muafaka na kutoa mrejesho kwa wafanyabiashara. Waziri Jafo amesisitiza kuwepo na mazingira bora Viwandani sababu kwa sehemu kubwa vinatoa ajira kwa vijana, na kuwawezesha kujikimu na kuongeza mafanikio katika sekta ya Viwanda. Ameyasema hayo Februari 10,2025 katika Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam uliowakutanisha Wanachama wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda Tanzania (CTI) na Viongozi wa Serikali Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdalah amesema Wafanyabiashara wako tayari kulipa kodi na wanahitaji kujua kiasi cha kodi kwanini wanalipa na kwa namna gani. Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila, ameeleza kuwa viongozi wa mkoa huo hawatakuwa kikwazo katika kutafuta suluhisho la changamoto hiyo na Mkoa wake uko tayari kushirikiana na sekta husika ili kuhakikisha mazingira ya biashara yanaboreshwa. Naye Mkurugenzi wa CTI), Bw. Leodegar Tenga, alisema kuwa ndani ya siku 60 wanatarajia kupata majibu yatakayosaidia sekta ya viwanda na uchumi kwa ujumla. Aidha amebainisha kuwa viwanda vina mchango mkubwa kwa serikali kupitia mapato na ajira, hivyo ni muhimu kutafuta suluhisho la tozo hiyo
0
1
2
Mabingwa watetezi Yanga wameshindwa kivuna point tatu dhidi ya maafande wa JKT Tanzania badala yake wameambulia point moja pekee baada kumaliza mchezo huo kwa suluu ya 0-0 Point hiyo moja kwa yanga inawafanya waendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na point 46. Yanga mechi ijayo wanatarajia kukutana na watoto wa kinondon KMC, mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Kmc Complex jijin Dar es Salaam. JKT Tanzania kwa sasa mesimama katika nafasi ya 9 ikiwa na alama zake 20 ambapo mchezo ujao inatarajia kucheza dhidi ya Singida Black Stars katika dimba la Mej Gen Isamuhyo.
0
1
3
Basi lililokuwa limebeba timu ya Dodoma limepata ajali hii leo Februari 10, 2025 katika eneo la kati ya Nangurunkuru na Somanga ambapo gari hilo lilidumbukia mtoni. Katibu Mkuu wa timu hiyo, Fortunatus Johnson amethibitisha tukio hilo akieleza kuwa wachezaji wote wamejeruhiwa kwa kukatwa na vioo vya gari. Dodoma jiji imepata ajaili hiyo wakati ikitokea mkoani lindi ambapo jana ilikuwa na mchezo dhidi ya Namungo fc, mchezo huo ulikamilikwa kwa sare ya 2-2.
0
1
4
Ni katika mechi ya leo ya round ya 18 ambayo Azm fc wamepoteza kwa kutandikwa bao 1-0 dhidi ya Wanalidanda Pamba jiji ya mwanza. Bao pekee lililoipa ushindi Pamba jiji limefungwa na Mchezaji Deus Kaseke mnamo dakika ya 88' ya mchezo. Ushindi huo kwa Pamba jiji unaifanya timu hiyo kufikisha pont 18 huku ikiwa tayari imecheza mechi 18 mpaka sasa. Azam fc mara baada yakupoteza mchezo huo inasalia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, ikiwa imekusanya alama 39 katika mechi 18 walizocheza.
0
1
2
Kylian Mbappe ameisaidia timu yake kupata point moja katika mechi ya Madrid Derby kati Real Madrid vs Atletico de Madrid Mechi hiyo iliomalizika kwa sare ya 1-1 imechezwa ndani ya uwanja wa nyumbani wa Real Madrid Santiago Bernabeu. Julian Alvarez aliitanguliza Atletico Madrid mapema dakika ya 35' kwa mkwaju wa Penalty, kabla ya Kylian Mbappe kusawazisha mnamo dakika ya 50' ya mchezo. Mbappe anafunga bao lake la 16 katika ligi ya Hispania tangu alipojiunga na Madrid, nyuma ya Lewandowski mwenye magoli 18.
0
1
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camilius Wambura, amesikitika kutangaza kifo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Beatus Silla wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania jijini Dodoma, kilichotokea Februari 7, 2025. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, SACP Silla alifariki dunia majira ya saa 11:00 asubuhi katika Taasisi ya Mifupa (MOI), jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu. Hata hivyo, sababu za kifo chake bado hazijawekwa wazi na Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi limeeleza masikitiko yake kwa familia, ndugu, jamaa na watumishi wote wa jeshi hilo kufuatia msiba huo, ratiba ya mazishi itatangazwa baadaye. @tanpol
0
1
1
Walipakodi mkoani Tabora wameahidi kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kulipa Kodi kwa hiari na kuwafichua Wafanyabiashara wanaokwepa Kodi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano baina yao na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda Wafanyabiashara hao wamesema wanajivunia kulipa Kodi kutokana na maendeleo makubwa yanayofanywa na serikali. Alex Mlifwe, Isihaka Yange na Shaban Muhinda ni miongoni mwa Wafanyabiashara waliozungumza kwenye mkutano huo na kuiomba TRA kuwafikia Walipakodi wengi zaidi hasa waliopo katika maeneo ya vijijini. Wamesema wapo watu wengi wanaofanya biashara bila kulipa Kodi Hali inayowaumiza wachache wanaolipa Kodi maana masoko wanayotumia ni ya aina moja na kushari wote wafikiwe. Akizungumza na Wafanyabiashara hao pamoja na kujibu baadhi ya hoja za Wafanyabiashara Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amewashukuru Walipakodi mkoani Tabora kwa kuendelea kuiunga mkono TRA kwa kulipa Kodi kwa hiari. Kamishna Mkuu Mwenda amesema kama ilivyo katika maeneo mengine amekutana na Wafanyabiashara hao kwa lengo la kuwashukuru na kusikiliza changamoto zao pia kuzipatia ufumbuzi ili kuweka mazingira rafiki katika ukusanyaji wa Kodi. Amesema Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan alimuagiza wakati akimuapisha kuwa asimamie ukusanyaji wa Kodi bila kutumia nguvu na ndicho anachokisimamia hali ambayo imeongeza makusanyo ya Kodi na kufanya TRA ivuke malengo ya makusanyo kwa kipindi cha miezi 7 mfululizo. Kuhusu watu wanaokwepa Kodi amewaomba Wafanyabiashara hao kushirikiana na TRA kuwafichua ili idadi ya walipakodi nchini iongezeke hali inayoweza kupunguza viwango vya Kodi. Kuhusu suala la Elimu kwa Mlipakodi Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA inaendelea kutoa elimu ili kuwezesha walipakodi kutambua wajibu wao na kujua walipe kiasi gani, walipe muda gani na kwa namna gani. @TRATanzania
0
1
0