![WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1590935212954894336/3U6C4-7r_x96.jpg)
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII
@maendeleoyajami
Followers
34K
Following
14K
Statuses
7K
Ukurasa rasmi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum S.L.P 573 Dodoma, Tanzania :Official page for MoCDGWSG
Dodoma, Tanzania
Joined July 2017
#MatukioKatikapicha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amezindua Kituo cha Huduma Jumuishi za Msaada kwa Manusura wa Ukatili (One Stop Center (OSC) katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime, mkoani Mara, leo Februari 8, 2025. Kituo hicho kimejengwa na Serikali kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Jinsia na Uzazi (UNFPA) lililochangia kiasi cha Shilingi 186,864,291.00, ambazo zimetumika kwa ujenzi wa jengo hilo pamoja na ununuzi wa samani na vifaa muhimu vya kutoa huduma. Uzinduzi huu umefanyika wakati wa kuhitimisha Maadhimisho ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji Duniani, ambapo Waziri Dkt. Gwajima alikuwa mgeni rasmi. Kituo hiki kitatumika kutoa huduma za haraka na za pamoja kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia, ikiwemo huduma za afya, ushauri wa kisaikolojia, msaada wa kisheria, na ulinzi wa polisi. Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, ukeketaji, na unyanyasaji wa wanawake na watoto wa kike, kwa kuhakikisha waathirika wanapata msaada kwa wakati. "Imarisha Ushirikiano, Tokomeza Ukatili!"
2
8
8
SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU, VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII. Na WMJJWM-Iringa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kujikita katika ukarabati wa miundombinu chakavu na ujenzi wa miundombinu mipya na ya kisasa kwa ajili ya taasisi za mafunzo nchini hususani Vyuo vya Maendeleo ya Jamii. Naibu Waziri Mwanaidi ameyasema hayo Februari 08, 2025 mkoani Iringa wakati akizindua jengo la Bwalo la Chakula katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha. Naibu Waziri Mwanaidi amesema Chuo cha Mendeleo ya Jamii Ruaha ni miongoni mwa Taasisi za mafunzo zilizonufaika na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali, ambapo ametoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Utawala, Bweni la Wasichana pamoja na Jengo la Kituo cha Ubunifu na Maarifa. Ameongeza kwamba, Serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili, maktaba, ukumbi wa mihadhara pamoja na bwalo la chakula la kisasa ambayo kwa pamoja yameongeza wigo wa utoaji wa huduma za elimu chuoni hapo. Amesema Mwaka 2022/23 Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo kwa lengo la kutatua changamoto iliyokuwa inawakabili wanafunzi ya kukosa sehemu nzuri ya kupatia huduma ya chakula. "Ninawasihi tuungane na kumpongeza Mheshimiwa Rais na Serikali yake sikivu kwa kuondoa kadhia iliyokuwa inawakabili wanafunzi kwa muda mrefu. Nina amini kuwa bwalo hili litaongeza tija ya kuinua taaluma ya Chuo hiki kwa kuwawezesha wanafunzi kupata huduma ya chakula katika mazingira salama, rafiki na kwa wakati" amesema Naibu Waziri Mwanaidi Mhe. Mwanaidi ametoa rai kwa Jumuiya ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha kuhakikisha kuwa wanatunza miundombinu yote ya Chuo hicho hususani bwalo la chakula na kuhakikisha lengo la Serikali la kujenga miundombinu rafiki ya kutolea huduma ya elimu kwa Wananchi linatimia kikamilifu kama ilivyokusudiwa. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Doris Kalasa ameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kukiwezesha Chuo hicho kuboresha miundombinu mbalimbali inayohusika na kujifunza na kujifunzia ili kuendana na mabadiliko ya utoaji wa elimu hasa katika mabadiliko ya Teknolojia. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha Godfrey Mafungu amemuhakikishia Naibu Waziri Mwanaidi kuwa atasimamia vyema utunzaji wa miundombinu mbalimbali Chuoni hapo ili idumu na kunufaisha wanafunzi watakaosoma vizazi kwa vizazi.
0
0
1
#Video Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mara, Wilaya ya Tarime pamoja na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili, wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake na Watoto wa Kike mnamo Februari 6, 2025, wilayani Tarime mkoani Mara.
0
0
1
VIONGOZI NA WADAU MKOA WA MARA WAJA NA MKAKATI MADHUBUTI WA KUKOMESHA UKEKETAJI Na WMJJWM - Mara Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mara, Wilaya ya Tarime pamoja na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili, wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake na Watoto wa Kike mnamo Februari 6, 2025, wilayani Tarime mkoani Mara. Katika maadhimisho hayo wadau walijadili mikakati madhubuti ya kutokomeza ukatili wa kijinsia, hususan ukeketaji, ambapo wamependekeza hatua kadhaa zitakazosaidia kuwalinda watoto wa kike dhidi ya ukatili huo. Miongoni mwa mapendekezo ni kuanzishwa kwa programu maalum mashuleni zitakazotoa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji kwa mtoto wa kike na jamii kwa ujumla ili kukuza uelewa na kuondoa mila hii potofu. Vilevile, ilipendekezwa kuwepo kwa adhabu kali zaidi kwa yeyote atakayebainika kushiriki katika vitendo vya ukeketaji. Mkuu wa Polisi Jamii wa Tarime-Rorya, ACP Jumanne Mkwama amebainisha kuwa katika mwaka 2024 pekee, jumla ya kesi 1,131 za ukatili wa kijinsia ziliripotiwa katika Dawati la Jinsia na Watoto wilayani humo. Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi limeongeza juhudi za kudhibiti matukio hayo. Aidha, ACP Mkwama amesisitiza kuwa jamii haipaswi kufumbia macho matukio ya ukatili, akiongeza kuwa kwa mwaka 2025, polisi wamejipanga kutoa elimu zaidi kwa wazazi, wazee wa kimila, na jamii kwa ujumla kuhusu madhara ya ukeketaji ili kuongeza mwamko wa kuripoti vitendo hivyo na hatimaye kuvimaliza kabisa. Kwa upande wake, Mratibu wa Kampeni ya Kutokomeza Ukeketaji nchini, Denis Moses, ameeleza kuwa ushirikiano wa jamii nzima—ikiwemo watoto, wazazi, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, wazee wa mila, na viongozi wa dini ni msingi imara wa kufanikisha mapambano dhidi ya ukeketaji. Naye Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Mara, Elizabeth Mhenya amesema kuwa Mkoa wa Mara umejipanga kuendelea kupunguza na hatimaye kutokomeza ukeketaji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu kwa jamii, kuendesha kampeni za uhamasishaji, na kuongeza juhudi za kupinga ukatili wa kijinsia. "Nawashukuru wote mlioleta mapendekezo kuhusu njia bora za kukomesha ukeketaji. Tumeyapokea na tutayafanyia kazi. Ingawa bado tunakabiliana na changamoto, tumejipanga kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa vitendo hivi vya ukatili," amesema Elizabeth.
0
0
0
#Matukiokatikapicha Leo Februari 6, 2025 ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake na Watoto wa Kike ambapo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeadhimisha siku hii wilayani Tarime mkoani Mara kwa kupaza sauti ya kupiga vitendo ya kutokomeza ukeketaji na kulinda haki za Wanawake na Watoto wa kike pamoja na kuhimiza jamii kutoa taarifa dhidi ya wanaojihusisha na vitendo vya ukeketaji kwa manufaa ya vizazi vya baadaye. "Imarisha Ushirikiano; Kutokomeza Ukeketaji" @maendeleoyajami @ortamisemitz @Sheria_Katiba
@UNFPATanzania
@SemaTanzania
@ElimikaWikiendi
@SuomiFinlandFTW
@Kehongoh_Marwa
0
1
1
#malezichanya "Mzazi na Mlezi, Je wajua unaweza kusikiliza na kuheshimiwa kwenye familia bila kufanya vitendo vya kikatili? Usalama na Ustawi wa Jamii unaanza na wewe." Katibu Mkuu Wizara ya @maendeleoyajami Dkt. @JohnJingu1
1
8
14
Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji Februari 06, 2025. Kauli Mbiu "Imarisha Ushirikiano; Kutokomeza Ukeketaji. Fahamu nani anawafanyia Wanawake na Watoto wa kike Ukatili wa Ukeketaji. @maendeleoyajami @ortamisemitz @Sheria_Katiba
@UNFPATanzania
@SemaTanzania
@ElimikaWikiendi
@SuomiFinlandFTW
@Kehongoh_Marwa
0
8
8
Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji Februari 06, 2025. Kauli Mbiu "Imarisha Ushirikiano; Kutokomeza Ukeketaji. Ijue Mikoa ambayo kiwango cha Ukeketaji kimeongezeka kati ya Mwaka 2015/16 hadi 2022/23 @maendeleoyajami @ortamisemitz @Sheria_Katiba
@UNFPATanzania
@SemaTanzania
@ElimikaWikiendi
@SuomiFinlandFTW
@Kehongoh_Marwa
0
2
6
Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji Februari 06, 2025. Kauli Mbiu "Imarisha Ushirikiano; Kutokomeza Ukeketaji. Ijue Mikoa ambayo imefanya kazi kubwa kupunguza Ukeketaji kati ya Mwaka 2015/16 hadi 2022/23 @maendeleoyajami @ortamisemitz @Sheria_Katiba
@UNFPATanzania
@SemaTanzania
@ElimikaWikiendi
@SuomiFinlandFTW
@Kehongoh_Marwa
0
3
2
Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji Februari 06, 2025. Kauli Mbiu "Imarisha Ushirikiano; Kutokomeza Ukeketaji. Ijue Mikoa 10 inayofanya vitendo vya Ukeketaji. @maendeleoyajami @ortamisemitz @Sheria_Katiba
@UNFPATanzania
@SemaTanzania
@ElimikaWikiendi
@SuomiFinlandFTW
@Kehongoh_Marwa
0
2
1
Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji Februari 06, 2025. Kauli Mbiu "Imarisha Ushirikiano; Kutokomeza Ukeketaji. @maendeleoyajami @ortamisemitz @Sheria_Katiba
@UNFPATanzania
@SemaTanzania
@ElimikaWikiendi
@SuomiFinlandFTW
@Kehongoh_Marwa
0
3
3
TAARIFA MUHIMU: Vitenge vya Siku ya Wanawake Duniani 2025 vinapatikana kwa bei ya shillingi 25,000 kwa jumla na Shillingi 30,000 kwa rejeareja katika Ofisi za Afiki Design Jengo la Derm Plaza Makumbusho Dar Es Salaam kwa Mawasiliano piga simu namba 0678781476. Kibango cha pili ni Wasambasaji katika Mikoa mbalimbali NB: Kwa wanaohitaji kusambaza Vitenge katika Mikoa tafadhali wasiliana na Msambazaji Mkuu kwa namba hapo juu.
0
5
7
4. Nukuu ya Waziri wa @maendeleoyajami Mhe. @Dr_DGwajima kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025
1
1
1
3. Nukuu ya Waziri wa @maendeleoyajami Mhe. @Dr_DGwajima kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025
0
0
0
2. Nukuu ya Waziri wa @maendeleoyajami Mhe. @Dr_DGwajima kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025
0
0
0
1. Nukuu ya Waziri wa @maendeleoyajami Mhe. @Dr_DGwajima kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025
0
0
0