ortamisemitz Profile Banner
OFISI YA RAIS TAMISEMI Profile
OFISI YA RAIS TAMISEMI

@ortamisemitz

Followers
66K
Following
81
Statuses
8K

Ukurasa Rasmi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, (Official Page for PO-RALG) https://t.co/k3ENeUVQHe 1923 Dodoma Email: [email protected] Mji wa Serikali Mtumba

Dodoma, Tanzania
Joined October 2020
Don't wanna be here? Send us removal request.
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
8 hours
MENEJA TARURA KILIMANJARO AAGIZWA UKARABATI BARABARA YA SONU-SAWE Naibu Waziri wa @ortamisemitz Mhe. Dkt. Festo Dugange, amemuelekeza Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Kilimanjaro kuwasilisha maombi maalumu ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Sonu kwenda Sawe ambayo imeharibika kutokana na mvua. Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo Februari 10, 2025 alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe aliyetaka kujua ni lini serikali itakarabati barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote. Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Dkt. Dugange alisema: "Namuelekeza Meneja wa TARURA mkoa wa Kilimanjaro na Meneja wa TARURA Wilaya ya Hai, kama hawajawasilisha maombi maalumu na tathmini ya mahitaji ya fedha, wafanye hivyo mara moja ili serikali ipeleke fedha kwa ajili ya kuirekebisha barabara hiyo." Katika swali la msingi, Mbunge wa Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo, amehoji lini serikali itapeleka fedha za dharura wilayani Kishapu kwa ajili ya matengenezo ya barabara zilizoathiriwa na mvua za El Nino mwaka 2023/24. Dkt. Dugange akijibu swali hilo, amefafanua kuwa serikali tayari imepeleka sh. milioni 190 katika mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya matengenezo ya dharura kwenye baadhi ya maeneo, ikiwemo barabara ya Mwamakanga – Mwanghiri yenye urefu wa kilomita 4.5 pamoja na ujenzi wa makalavati saba. Aidha, ameeleza kuwa TARURA Wilaya ya Kishapu inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 1,024.66, ambapo kilomita 2 ni za lami, kilomita 405.64 ni za changarawe, na kilomita 617.02 ni za udongo. Katika tathmini ya mwaka 2023/24, serikali ilibaini kuwa Sh.Bilioni 2.55 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo. Dkt. Dugange amesisitiza kuwa serikali itaendelea kutekeleza matengenezo ya barabara zote zilizoathiriwa na mvua, kulingana na upatikanaji wa fedha. &&&&
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
1
5
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
10 hours
MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA ZA TACTIC MOROGORO ATAKIWA KUKAMILISHA KAZI NDANI YA MIEZI MITATU Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemtaka Mkandarasi M/s Jiangxi GEO Engineering Group anayejenga barabara ya Kihonda - VETA yenye urefu wa Km 12.85 kwa kiwango cha lami Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa ubora unaotakiwa ndani ya miezi mitatu hadi kufikia mwezi Mei 2025. Mhandisi Mativila ametoa agizo hilo kwa mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa mradi huo katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo unaotekelezwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTIC) chini ya mkopo nafuu toka Benki ya Dunia. “Nimekuja kutembelea moja ya miradi mikubwa ambayo serikali ya awamu ya sita inatekeleza kwa ajili ya kuleta maendeleo na ushindani katika miji 45 ya Tanzania iliyochanguliwa iwe na ushindani wa kuwa na miundombinu bora ikiwemo ya barabara kwa kiwango cha lami inayowezesha kukua kwa uchumi’’, alisema. Alisema kati ya miji hiyo ni pamoja na Manispaa ya Morogoro ambayo inanufaika na utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambapo kwa mkoa huo mradi unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 19.6. “Mradi huu umechelewa na upo nyuma kwa asilimia 18 na kwamba umetekelezwa kwa asilimia 82 tu na kuna sababu kadhaa ambazo zimeelezwa, baada ya kuweka mambo sawa tunataka mradi huu ukamilike ndani ya muda wa miezi mitatu endapo kukiwa na mvua kubwa basi mradi uwe umekamilika Mwezi Augosti mwaka huu“, alisema . Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Mohamed Muanda alisema ujenzi wa mradi huo ulianza Oktoba 23, 2024 na kutakiwa kukamilika Februari 2025 ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji ya mvua kuelekea mto Kikundi yenye urefu wa jumla ya Km 4.4, ujenzi wa ofisi ya Mhandisi Mshauri na ofisi ya wasimamizi wa miradi. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mhandisi Mshauri kutoka nchini pamoja na Mhandisi Mshauri kutoka Ethiopia (JV Core consultancy), Mhandisi Dargie Dilbedi alimhakikishia Naibu Katibu kwamba kazi hiyo ipo katika hatua ya mwisho na kwamba anatumaini ndani ya miezi mitatu ya nyongeza itakamilika. Mwisho.
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
0
5
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
11 hours
0
0
3
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
15 hours
Tweet media one
3
26
68
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
19 hours
KAMATI YA BUNGE YAELEKEZA HALMASHAURI ZENYE MAPATO MAKUBWA KUJENGA UZIO MAENEO YA HUDUMA ZA AFYA Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, imeielekeza Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuhakikisha Halmashauri zote nchini zenye mapato makubwa ya ndani zinajenga uzio katika maeneo ya kutolea huduma za afya kwa ajili ya usalama wa wananchi na mali za umma. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga ametoa maelekezo hayo wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya elimu na afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Mkoa wa Pwani. “Tukipita kwenye maeneo mengi tunaona hospitali hazina uzio. Kutokana na maeneo mengi kuwa karibu na makazi ya watu, Kamati inashauri Halmashauri zenye mapato ya ndani ya kutosha zianze kujenga uzio kwenye maeneo ya huduma za jamii kama haya,” amesema Mhe. Nyamoga. Ameongeza kuwa ni muhimu maeneo yanayotoa huduma za afya kuwa salama na kuhakikisha faragha kwa wagonjwa na wateja wanaoingia na kutoka. Pamoja na hilo, Mhe. Nyamoga amezitaka Halmashauri zote nchini kufuata miongozo na taratibu katika matumizi ya fedha za miradi ya BOOST na SEQUIP, ili Watanzania waendelee kunufaika na juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya elimu. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, amepokea maelekezo hayo huku akisisitiza umuhimu wa Halmashauri kuendeleza miundombinu katika sekta nyeti, ikiwamo sekta ya afya. Kamati hiyo imemaliza ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Pwani, ambapo imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Rufiji na Manispaa ya Kibaha. &&&
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
12
30
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
1 day
0
1
3
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
1 day
0
10
34
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA RUFIJI KWA UTEKELEZAJI BORA WA MIRADI OR-TAMISEMI KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Rufiji, hususan ukarabati wa Hospitali ya Wilaya pamoja na miradi mingine ya afya, elimu, miundombinu na masoko. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Justin Nyamoga ameyasema hayo atika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, soko, jengo la utawala na miundominu ya barabara za TARURA inayotekelezwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI. Mhe. Nyamoga amepongeza usimamizi mzuri wa miradi hiyo, akibainisha kuwa Rufiji imeonyesha mfano bora wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo. "Mhe. Waziri, tumejionea kazi nzuri ya ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Rufiji. Tumefurahishwa na ubora wa mradi huu, hivyo tunakupongeza kwa usimamizi mzuri. Rufiji ni mfano wa kuigwa," amesema Mhe. Nyamoga. Aidha, Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Salome Makamba, ameeleza kuwa licha ya hospitali hiyo kujengwa mwaka 1963, ukarabati wake umefanyika kwa kiwango cha hali ya juu, jambo linaloonyesha utekelezaji mzuri wa miradi ya serikali. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu), Mhe. Zainab Katimba, ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, serikali imewekeza zaidi ya Sh.Trilioni 1.2 katika sekta ya afya, huku Rufiji pekee ikinufaika na uwekezaji wa Sh.Bilioni 8.3. Mbunge wa Jimbo la Rufiji, ambaye pia ni Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ameeleza kuwa pamoja na maboresho ya huduma za afya, Rufiji inaendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwamo ujenzi wa kiwanda kikubwa cha sukari, kiwanda cha ndizi kinachotarajiwa kutoa ajira zaidi ya 8,000, pamoja na ujenzi wa bandari ndogo ya Muhoro kwa ajili ya kusafirisha bidhaa za kilimo. Ziara ya Kamati hiyo wilayani Rufiji ilihitimishwa kwa ukaguzi wa miradi mbalimbali, ikiwamo soko la Umwe, jengo la Halmashauri ya Mji, barabara za TARURA, na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Pwani – Bibi Titi Mohamed. &&&&
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
13
31
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
VIJANA WENYE UMRI HADI MIAKA 45 SASA KUNUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI Naibu Waziri wa @ortamisemitz anayeshughulikia Afya, Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa ukomo wa umri wa vijana wanaostahili kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri umeongezwa kutoka miaka 35 hadi 45. Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Bunda, Mhe. Boniphace Mwita Getere aliyetaka kujua ni lini Serikali itatenga dirisha maalum la mikopo kwa wanaume waliovuka umri wa vijana. Akijibu swali hilo, Dkt. Dugange ameeleza kuwa mikopo hiyo ya asilimia 10 hutolewa kwa makundi maalum ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kwa masharti nafuu bila riba, kwa kuwa makundi hayo yana changamoto ya kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha kutokana na ukosefu wa dhamana na uwezo wa kumudu riba kubwa. "Ukomo wa umri wa vijana wanaostahili kupata mikopo sasa umeongezwa kutoka miaka 35 hadi 45," amesema Dkt. Dugange. Katika swali la nyongeza, Mhe. Getere amehoji ni lini Serikali itatoa mwongozo rasmi kwa Halmashauri ili wananchi wa vijijini wapate ufahamu kuhusu mabadiliko hayo. Dkt. Dugange amefafanua kuwa baada ya kukamilika kwa kanuni za mikopo ya asilimia 10 za mwaka 2024, tayari miongozo imeshatolewa na kusambazwa kwa Halmashauri zote 184. Amesisitiza kuwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 45 sasa wanastahili mikopo hiyo, huku akitoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi ili kuongeza idadi ya wanufaika. &&&&
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
1
23
45
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeanza ziara ya kikazi mkoani Pwani tarehe 08.02.2025 na katika siku ya kwanza Kamati imetembelea Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji. Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Justine Nyamoga ameongoza ziara hiyo katika Wilaya ya Rufiji kutembelea na kukagua ukarabati wa hospitali ya Wilaya hiyo, shule maalum ya wasichana ya sayansi ya wanawake ijulikanayo kama Bibititi Mohamed, ujenzi wa jengo la utawala pamoja na ujenzi wa soko. Ziara hiyo inaendelea katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani.
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
13
26
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
Tuzo ‘Tuzo imetolewa kwa Mhe. Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa usimamizi wa utekelezaji wa mfumo wa Anwani za Makazi katika ngazi zote yaan Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa’ Tuzo hii imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi - 2025 na kupokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange kwa niaba ya Mhe. Mchengerwa.
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
6
13
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA ZA TACTIC JIJINI DODOMA ATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI KWA WAKATI Dodoma Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemuagiza Mkandarasi M/s China Geo-Engineering Corporation kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa barabara kiwango cha lami Km 10.21, mtaro wa maji ya mvua Ilazo Km 2.1, uboreshaji wa mabwawa ya kuhifadhi maji ya mvua (3), mitaro ya kutiririsha maji Km 2.81 pamoja na ujenzi wa jengo la usimamizi na uratibu wa miradi kwa wakati na ubora. Mhandisi Mativila ametoa agizo hilo alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo jijini Dodoma ambayo inatekelezwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTIC) chini ya mkopo nafuu toka Benki ya Dunia. Naibu Katibu Mkuu ameeleza kuwa baada ya ukaguzi wa mradi huo amebaini kuwa ujenzi wa barabara, mifereji ya maji ya mvua pamoja na jengo la usimamizi na uratibu wa miradi upo nyuma ya muda kutokana na nguvu kazi hafifu, ukosefu wa vitendea kazi na kupelekea mradi huo ambao unapaswa kukamilika Februari 2025 kuonyesha ishara za kutofikia malengo ya kukamilika kwa muda na kuwanyima wananchi fursa ya kupata huduma ya barabara. “Mradi upo asilimia 45% tu bado zimebaki 55% kazi kukamilika, mpaka leo zimebaki siku 13 tu ili mkataba ukamilike. Tumeongea na mkandarasi lakini tumeona sehemu kubwa ya ucheleweshaji wa kazi umesababishwa na mkandarasi mwenyewe kwa kushindwa kuweka nguvu kazi na vifaa vya kutosha, ametueleza anahitaji mwaka mwingine ili akamilishe kazi kiukweli ataongezewa muda lakini atapata adhabu ya kukatwa fedha kulingana na mkataba na pia atatakiwa afanye kazi usiku na mchana ili akamilishe kazi ndani ya muda mfupi na kwa ubora ule ule”. amesema
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
1
22
43
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA ANWANI ZA MAKAZI Dodoma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) alipotembelea banda la maonesho la @ortamisemitz na TARURA wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi leo tarehe 07 Februari, 2025 katika ukumbi wa Jakaya Convention Centre jijini Dodoma.
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
5
11
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali wakifuatilia matukio wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya anwani za makazi katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikua ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 08.02.2025!
Tweet media one
Tweet media two
0
7
23
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
ANWANI ZA MAKAZI ZABORESHA USAFIRISHAJI WA DAWA NA VIFAA VYA SHULE NCHINI OR - TAMISEMI Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Dkt. Festo Dugange, amesema kuwa mfumo wa anwani za makazi umeleta mapinduzi makubwa katika usambazaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini, kwani hakuna tena changamoto ya kutafuta au kuuliza eneo la zahanati au kituo cha afya kilipo. Akizungumza leo Februari 8, 2025 kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Anwani za Makazi jijini Dodoma, Dkt. Dugange ameeleza kuwa pamoja na dawa, mfumo huu pia umewezesha vifaa na mahitaji muhimu ya shule kufikishwa katika maeneo husika kwa ufanisi mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya utekelezaji wa mfumo huo. Aidha, amebainisha kuwa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) sasa inasambaza dawa moja kwa moja hadi kwenye zahanati katika maeneo yote ya Tanzania kwa kutumia anwani za makazi, jambo ambalo limeimarisha usambazaji wa dawa na huduma za afya kwa wananchi wa mijini na vijijini kwa kiwango kikubwa. Dkt. Dugange amesisitiza kuwa mfumo wa anwani za makazi umewezesha maeneo yote nchini kufikika kwa urahisi zaidi, na Ofisi ya Rais - TAMISEMI itaendelea kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wake unazidi kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. &&&&
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
0
13
31
@ortamisemitz
OFISI YA RAIS TAMISEMI
2 days
MHE.MCHENGERWA AONYA VIKUNDI HEWA MIKOPO YA 10% OR-TAMISEMI WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Mohamed Mchengerwa amesema Mkuu wa Mkoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa watakaobainika maeneo yao kuwa na vikundi hewa kwenye mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu watawajibishwa. Aidha, zaidi ya Sh.Bilioni 234 zinakusudiwa kupelekwa kwa wananchi kwa njia mbili za utoaji mikopo hiyo ambazo ni kupitia Benki kwa Halmashauri 10 na mikopo iliyoboreshwa kwenye Halmashauri 174. Akizungumza Februari 7, 2025 jijini Dodoma kwenye hafla ya utiaji saini mikataba kati ya Halmashauri 10 na Benki tatu ya utoaji mikopo hiyo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani, Mhe. Mchengerwa amesema kila mmoja afuatilie fedha hizo kuhakikisha zikishuka kama ilivyokusudiwa kwa walengwa ili zitabadili maisha yao. Amesisitiza uadilifu wa kwenye fedha hizo na kufuatilia kwa kina vikundi vyote na kuvijua na asisikie vikundi hewa. “Fedha hizi ni za moto wajibu wetu ni kumsaidia Rais fedha hizi zisiende kuchezewa, naelekeza kikundi hewa kitakachobainika eneo lolote viongozi wa eneo hilo mtapaswa kuwajibika, tumieni vyombo mnavyosimamia kwenye mikoa na wilaya kuhakikisha hakuna vikundi hewa, fedha zisimamiwe na kurejeshwa." “Nazielekeza Mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kuchangia fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo hii kwa mujibu wa sheria ya fedha za serikali za mitaa, na Katibu Mkuu niletee orodha kama kuna halmashauri ambazo hazijachangia na zinadorora kuchangia na kama kuna halmashauri ambayo haijatekeleza maelekezo ya Rais,”amesema. Amesema Benki ya NMB itafanya kazi kwenye halmashauri za wilaya za Bumbuli, Itilima, Newala, Manispaa ya Songea, Jiji la Dodoma na Jiji la Dar es salaam huku benki ya CRDB itafanya kazi Wilaya za Nkasi, Mji wa Mbulu, Manispaa ya Kigoma, Jiji la Dar es salaam na Jiji la Dodoma na Benki ya Biashara ya Uchumi itafanya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Siha. Awali, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Adolf Ndunguru amesema kusainiwa mikataba hiyo ni mwanzo wa mapinduzi ya kuhakikisha mikopo hiyo ya asilimia 10 inakuwa na tija tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. &&&&
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
10
32
74