![Zahoro Muhaji Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1551084189050707968/EAXtvExX_x96.jpg)
Zahoro Muhaji
@ZMuhaji
Followers
8K
Following
23K
Statuses
14K
Ordinary person. Among the founders and CEO for @TanzaniaSA. My mantra “There is a World out there”. Wellbeing-Prosperity- The pursuit of Happiness.
Tanzania
Joined October 2014
Rest in easy brother @DocFaustine you are missed!
A heartfelt tribute of @DocFaustine published in @TheLancet. Rest in Peace, my dear brother Faustine. You inspired so many of us with your vision for @WHOAFRO. You have left a legacy and vision for us to take forward.
0
0
1
RT @JaphetSayi: While PPP sounds like one of the best option literature and history do not always point to that direction. United Kingdom…
0
10
0
RT @TZStartupWeek: 🚀 JOIN THE TANZANIA STARTUP WEEK 2025 ORGANIZING COMMITTEE! 🚀 We’re looking for 11 dynamic leaders from Tanzania’s star…
0
3
0
Strive Masiyiwa, mmoja kati ya Waafrika mashuhuri ninaowaheshimu sana.
Jana nilipata fursa ya kuonana na Ndugu Strive Masiyiwa katika hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Taasisi ya Kings Trust International. Ndugu Masiyiwa ni mfanyabiashara maarufu barani Afrika anayemiliki Makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni ya mawasiliano ya Econet Group na Cassava Technologies. Vilevile Ndugu Masiyiwa ni mmoja wa washirika wa Taasisi ya Kings Trust International iliyoasisiwa na Mfalme Charles III wa Uingereza. Taasisi hiyo inaendesha programu mbalimbali za kuwajengea uwezo vijana kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi. Katika mazungumzo na Ndugu Masiyiwa- nilimueeleza kuwa nilimuona katika mkutano wa World Economic Forum uliofanyika Davos mwezi Januari 2025 ambapo alielezea kwa uchungu jinsi vijana wa Afrika walivyokuwa na mawazo mazuri na uwezo mkubwa wa kuanzisha na kuendesha biashara kama ilivyo vijana wa Ulaya na Marekani lakini changamoto yao kubwa ni ukosefu wa mitaji. Nilimuuliza kwa maoni yake- nini kifanyike kuziwezesha biashara zinazoanza (Startups) za Afrika kupata mitaji. Ndugu Masiyiwa alieleza kwamba mahala pa kuanzia kutafuta mitaji ya kuziwezesha Startups ni ndani ya Afrika kabla ya kufikiria kwenda nje. Kinachotakiwa ni kuwekwa sera za makusudi zitakazochochea mitaji ielekezwe kwenye Startups. Na mitaji yenyewe isiwe mikopo bali equity investment. Alishauri lazima nchi za Afrika ziweke sheria inayoilazimu Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima kuelekeza asilimia 5 ya uwekezaji wake katika Startups. Aidha, alieleza kuwa lazima juhudi za makusudi zifanyike kuhakikisha biashara hizo zinafanikiwa kwa kuzihakikishia masoko. Mfano zipo nchi ambazo zimeweka katika sheria inayoitaka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kuhakikisha asilimia 30 ya manumuzi ya huduma na bidhaa ifanyike kutoka katika Startups... na pale zinapoanzishwa zinapewa msamaha wa kodi kwa kipindi cha hadi miaka mitano ili zisimame na kuimarika kabla ya kuanza kulipa kodi. Na wale wanaozalisha bidhaa ndani ya nchi za Afrika lazima walindwe katika hatua za awali za biashara yao ili wasizifiwe na ushindani wa bidhaa zilizozalishwa katika viwanda vya nje. Kuruhusu bidhaa za nje kuingia kiholela ni sawa na kuwezesha viwanda vya nje kufanikiwa huku viwanda vya ndani vinavyotoa ajira kwa waafrika vikianguka. Hata CFTA iliyoanzishwa na mataifa ya Afrika lazima inufaishe wazalishaji wa Afrika kwanza. Tumekubaliana na Ndugu Masiyiwa tutakutana tena kuzungumzia suala hili muhimu kwa mustakabali wa Bara la Afrika. Ni matumani yangu katika mkutano kuhusu uwezeshaji wa Startups utakaofanyika jumatatu tarehe 10 Februari 2025 - zitazungumzwa mbinu za ndani na nje za kuzinyanyua Startups zetu
1
1
7
Kiutamaduni makabila na watu wa Pwani hakuna ukeketaji. Lakini kama ripoti inavyosema, kuna wimbi jipya katika mikoa hiyo, nadhani inachangiwa zaidi na uhamiaji wa makabila mengi haswa ya jadi ufugaji ambao wameingia sana mikoa ya Pwani kufuata malisho ya mifugo na ndio wana desturi hizo kutoka walikotoka.
1
1
1
RT @amour_maryam: Congratulations Dr @Chikwe_I on your appointment as acting @WHOAFRO Regional Director 👏👏👏
0
12
0
Habari za kuhuzunisha sana kusikia kifo cha Mwanahabari nguli @ahmedrajab. Nilifurahia sana kusoma makala zake zilizokua zimejaa historia nzuri ya nchi yetu, siasa na watu wake, tena kwa lugha nzuri sana ya Kiswahili chake cha mwambao. Mwenyezi Mungu akumpuzishe mahala pema peponi🙏🏿
0
5
18
Maamuzi ya magumu na ya busara sana. Sio rahisi sana kutengeneza Sera nchi hii, sababu sio rahisi kuuza utengenezaji wa Sera kama mafanikio. Kwa ujumla, vitu vinavyoonekana kama madaraja, barabara, reli vina mvuto kwa wapiga kura kuliko Sera. Lakini Sera ndio huamua Dira, maono, matamanio na muelekeo kwenye Taifa lolote. Hivyo Sera hii ya Elimu ikifuatwa ndio njia ya kwenda kuijenga Tanzania ya miaka 50 mbele. Hongera sana Mheshimiwa Rais @SuluhuSamia
Mapema leo katika kazi jijini Dodoma ambapo nchi yetu imeandika historia kwa kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023, pamoja na mitaala iliyoboreshwa katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu. Uamuzi huu wa kihistoria wa kuboresha sera na muundo wa elimu yetu unakusudia kulipa Taifa letu vijana wenye elimu bora zaidi, wanaojiamini zaidi, na wenye nyenzo stahiki kushindana kikanda na kimataifa. Kazi ya msingi ya ujenzi wa miundombinu inayobeba utekelezaji wa sera na mabadiliko haya inaendelea, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 tumejenga shule mpya za msingi 1,649, shule mpya za sekondari 1,042, vyuo 64 vya ufundi stadi (VETA) katika wilaya 64 ambazo awali hazikuwa navyo. Nimeelekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Mipango na Uwekezaji kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mabadiliko haya ili yaweze kuleta manufaa tunayokusudia. Utekelezaji huu uende sambamba na kupitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahili kama mama wa taaluma zote duniani.
0
1
6
RT @Prosper_absalom: Happy to announce we’re updating our @KuzaBusiness mobile with a whole new different experience. From booking to bank…
0
17
0
RT @elisha_bulalu: i’m building an intelligent driving agent —one that doesn’t just track, but trully understands. having context about th…
0
33
0