![MalisaGJ Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1833903817198313474/KcnbQ3VP_x96.jpg)
MalisaGJ
@MalisaGJ_
Followers
40K
Following
706
Statuses
504
Award winning Philanthropist || SBC Specialist || Human Rights Activist || Simba SC Die Hard Fan
Dar es Salaam, Tanzania
Joined August 2018
#dit_tanzania Huyu dogo amelipa ada. HADAIWI. Pigia mstari neno hadaiwi. Lakini amezuiwa kufanya mtihani kwa sababu kalipa nje ya muda. Mliweka January 24 iwe deadline ya kulipa ada, lakini yeye akalipa tar.26. Swali kwanini leo azuiwe kufanya mtihani wakati ada kalipa? Watu wengi wanaochelewa kulipa ada si kupenda kwao bali hali ngumu ya maisha. Unakuta mwanafunzi hana wazazi, na hana mkopo wa serikali. Anasoma kwa kuombaomba kwa ndugu. Amepata ada, amelipa na mmeipokea na kumpa risiti? Kwanini mnamzuia kufanya mtihani kisa alilipa nje ya deadline? Yani mtoto alazimike kurudia mwaka wakati ada amelipa? Hii sio sawa. CC: #professoradolfmkenda, #wizara_elimutanzania
68
79
395
Jana Mahakama kuu ilitoa uamuzi kwamba shauri la Dr.Slaa lirudishwe Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya taratibu za dhamana. Kwahiyo leo ilikua siku ya kuletwa Kisutu ili apatiwe dhamana, lakini upande wa Jamhuri umeshindwa kumfikisha mahakamani kwa madai ya kukosa gari ya kumtoa Segerea kwenda Kisutu.!
43
38
354
RT @KingPablotz: Sehemu ya Pili Maisha ya Brian Deacon Baada ya Filamu ya "Jesus" (1979) Je, wajua maisha ya Brian Deacon baada ya kuigiz…
0
108
0
Mahakama Kuu ya Tanzania, masijala kuu jijini Dar Es Salaam imegiza shauri la mwanasiasa Mkongwe Nchini Dr.Wilbroad Slaa lirejeshwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake. Shauri hilo lilipelekwa Mahakama kuu baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumnyima dhamana, na kumfanya Dr.Slaa kusota gereza la Segerea kwa zaidi ya wiki mbili sasa.!
21
48
437
Mwenyekiti wa Chadema Taiifa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha demokrasia nchini (TCD), Wakili Msomi Tundu Lissu, amefika Mahakama kuu, kumtetea Balozi Dr.Wilbroad Slaa anayeshtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo mitandaoni. Shauri hilo lilifika mahakama kuu baada ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumnyima dhamana Dr.Slaa. Lissu anaungana na jopo la Mawakili wengine akiwemo @PMadeleka, @dicksonmatata, @HekimaMwasipu1 na wengine katika shauri hilo lililopangwa kusikilizwa leo.!
13
84
585
Makamu Mwenyekiti wa Chadema (bara), @HecheJohn akimpa "bwana kicheche" haki yake ya kikatiba kwenye press ya leo wakati uongozi mpya ulipokabidhiwa ofisi.!
28
148
956
@PolisiTanzania, @PolisiTanzania, @PolisiTanzania nimewaita mara 3. Tafadhali acheni kujitafutia laana za rejareja. Kama haya madai ni ya kweli basi mmemkosea sana marehemu. Kifo cha Jumanne hakijasababishwa na watu wenye hasira kali kama taarifa yenu inavyosema, bali kimesababishwa na watu wawili (mume na mke) ambao walikua maboss zake. Mke amekiri kwamba yeye ndiye aliyemwagia Jumanne petrol na mumewe akawasha kiberiti. Na walimchomea nyumbani kwao. Yani walienda kumchukua Juma kwake saa 4 usiku, alikua amelala, wakamuamsha wakaenda nae hadi kwao. Walipofika wakafungua geti wakaingia ndani. Wakamtuhumu kuiba laki mbili, kisha wakamchoma moto. Hayo yote yamefanywa na mtu na mkewe. Sasa mnasemaje ni wananchi wenye hasira kali? Je mnataka kupindisha ukweli ili muwasaidie hao wauaji watoke? Kumbukeni Jumanne ameacha mke na watoto wawili. Mmoja bado ni mchanga. Machozi ya hao watoto yatakua laana kwa askari wote watakaohusika kubadili documents ili hao wauaji waachiwe. Polisi yeyote atakayepindisha ukweli wa jambo hili, atalaaniwa mpaka kizazi chake cha 4. Hayo si maneno yangu, ni maagizo ya MUNGU mwenyewe. Katika kitabu cha Kutoka 20:5(b) Mungu anasema "Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao" Kwahiyo tafadhali tendeni haki, msije kutia familia zenu kwenye laana kwa sababu ya tamaa za muda mfupi. Kimsingi hiyo ni "murder" maana wameua kwa kukusudia. Elements zote za jinai zipo (actus reus and mens rea), yani nia ovu na tendo ovu. Kilichobaki ni nyie kukamilisha ushahidi ili hao wauaji wafikishwe mahakamani na wapewe haki yao ya kikatiba. Narudia kuwakumbusha maneno ya Mungu kwamba laana inaenda hadi kizazi cha 4. Usije ukaiweka familia yako, watoto wako, wajukuu zako na vitukuu vyako kwenye mnyororo wa laana kwa sababu ya tamaa zako za muda mfupi. Tenda haki utabarikiwa wewe na vizazi vyako. Mwenye masikio na asikie.!
0
0
1
@PolisiTanzania , @PolisiTanzania, @PolisiTanzania nimewaita mara 3. Tafadhali acheni kujitafutia laana za rejareja. Kama haya madai ni ya kweli basi mmemkosea sana marehemu. Kifo cha Jumanne hakijasababishwa na watu wenye hasira kali kama taarifa yenu inavyosema, bali kimesababishwa na watu wawili (mume na mke) ambao walikua maboss zake. Mke amekiri kwamba yeye ndiye aliyemwagia Jumanne petrol na mumewe akawasha kiberiti. Na walimchomea nyumbani kwao. Yani walienda kumchukua Juma kwake saa 4 usiku, alikua amelala, wakamuamsha wakaenda nae hadi kwao. Walipofika wakafungua geti wakaingia ndani. Wakamtuhumu kuiba laki mbili, kisha wakamchoma moto. Hayo yote yamefanywa na mtu na mkewe. Sasa mnasemaje ni wananchi wenye hasira kali? Je mnataka kupindisha ukweli ili muwasaidie hao wauaji watoke? Kumbukeni Jumanne ameacha mke na watoto wawili. Mmoja bado ni mchanga. Machozi ya hao watoto yatakua laana kwa askari wote watakaohusika kubadili documents ili hao wauaji waachiwe. Polisi yeyote atakayepindisha ukweli wa jambo hili, atalaaniwa mpaka kizazi chake cha 4. Hayo si maneno yangu, ni maagizo ya MUNGU mwenyewe. Katika kitabu cha Kutoka 20:5(b) Mungu anasema "Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao" Kwahiyo tafadhali tendeni haki, msije kutia familia zenu kwenye laana kwa sababu ya tamaa za muda mfupi. Kimsingi hiyo ni "murder" maana wameua kwa kukusudia. Elements zote za jinai zipo (actus reus and mens rea), yani nia ovu na tendo ovu. Kilichobaki ni nyie kukamilisha ushahidi ili hao wauaji wafikishwe mahakamani na wapewe haki yao ya kikatiba. Narudia kuwakumbusha maneno ya Mungu kwamba laana inaenda hadi kizazi cha 4. Usije ukaiweka familia yako, watoto wako, wajukuu zako na vitukuu vyako kwenye mnyororo wa laana kwa sababu ya tamaa zako za muda mfupi. Tenda haki utabarikiwa wewe na vizazi vyako. Mwenye masikio na asikie.!
0
0
0
RT @mshambuliaji: Watanzania waliokwama kwenye vita nchini Congo (DRC) wakiomba msaada baada ya waasi wa kikundi cha M23 kinachoungwa mkono…
0
300
0
Ulimwengu uliojaa UKATILI. Nimeambiwa Jumanne alikua mfanyakazi (gardener) kwenye nyumba moja hapo Kimara. Amefanya kazi kwa miezi kadhaa bila kulipwa mshahara wake. Akaamua kuacha kazi lakini akawa anadai pesa zake za miezi aliyofanya kazi. Tajiri akawa anamzungusha tu. Jana saa 4 usiku tajiri akatuma vijana nyumbani kwa Jumanne wakamwambia akachukue hela yake. Jumanne akamwacha mkewe na mtoto akaenda kufuata hela. Walipofika nyumbani kwa tajiri wakaanza kumpiga wakidai aliwaibia laki mbili alipokua akifanya kazi kwao. Jumanne akakanusha madai hayo, lakini akasema kama wanahisi amewaibia basi wamkate kwenye mishahara anayowadai. Hawakujali utetezi wake. Wakamfunga miguu na mikono kwa kamba. Wakamwagia petrol kisha wakamchoma moto. Halafu wakapiga kelele kujifanya mwizi kachomwa moto na wananchi wenye hasira 😭. Nimesikitika sana. Yani unamtumikisha mtu kwa miezi kadhaa bila malipo. Baadae unaona njia ya kukwepa deni ni kumuua? Tena kifo cha kikatili cha kumchoma moto? Halafu unamsingizia amekuibia laki mbili. Si ungemkata kwenye mishahara anayokudai? Imagine mke wake na mwanae wameshuhudia baba yao akichukuliwa saa 4 usiku. Wakapata matumaini kwamba baba anaenda kulipwa hela zake hivyo familia itapata neema. Lakini badala ya neema imekuja balaa. Baba hakurudi, badala yake umerudi mwili ulioungua na kuteketea kwa moto 😭. Hebu tafakari "trauma" atakayopitia huyu mtoto kwenye kukua yake? Amewekewa kumbukumbu mbaya ambayo haitakaa ifutike maisha yake yote. Kila atakapomkumbuka baba yake atakumbuka ile siku aliyochukuliwa na hakurudi tena, ukarudi mwili ulioteketea kwa moto 😭😭. Aisee hawa wauaji walaaniwe. Nalipongeza jeshi la @polisi.tanzania kwa kuwakamata washukiwa. Tafadhali wapeni haki yao ya kikatiba na muwafikishe mahakamani haraka iwezekanavyo. Ukatili huu ni wa kulaaniwa na kila mtu. Ukikaa kimya kesho inaweza kumkuta ndugu yako, rafiki yako, mwanao au baba yako. Naomba serikali ione namna ya kumsaidia mjane na mtoto aliyeachwa. This is so heartbreaking. R.I.P Jumanne 😭😭😭
265
220
1K
Anaandika Wakili Msomi @Mwabuk2Boniface Rais wa chama cha Mawakili nchini. __________ Kwa Tanzania, kwa mujibu wa sheria, mtu ana uhuru wa kutumia na kudhibiti mali yake anayoimiliki kihalali. Hata hivyo, suala la kuharibu mali yako kwa makusudi linaweza kuleta changamoto kisheria katika hali fulani: 1. Madhara kwa Jamii au Wengine: Iwapo uharibifu wa mali yako unaweza kusababisha madhara kwa watu wengine au mazingira, basi unaweza kuhusika kisheria. Kwa mfano, kuharibu mali kwa moto mahali ambapo kuna hatari ya kusababisha moto kusambaa au madhara kwa majirani, inaweza kuchukuliwa kama kosa la jinai. 2. Mikataba au Deni: Ikiwa mali hiyo imewekwa rehani au ni sehemu ya mkataba fulani (kama mkopo kutoka benki), kuharibu mali hiyo kwa makusudi kunaweza kuwa kosa kisheria. Benki au mdai mwingine anaweza kufungua kesi kwa sababu ya kuathiri dhamana ya deni. 3. Sheria za Mazingira: Ikiwa uharibifu wa mali yako unakiuka sheria za mazingira, unaweza kushtakiwa kwa mujibu wa sheria hizo. Kwa kifupi, ingawa mtu ana haki ya kutumia mali yake, haki hiyo siyo ya kibinafsi kabisa ikiwa inagusa maslahi ya umma, watu wengine, au haki ya mkataba. Kimsingi kama umepewa Kitu na Mtu na Ukakipokea na ikafika wakati hukihitaji tena, basi wape wengine kitu hicho. Kuharibu, kuchoma au kufanya jambo lolote lile kwa namna ya dhihaka ni kumfanya Mungu kuwa dhaifu, na huo ni Ushirikina. JEHOVA siyo Dhaifu tuache ushirikina. Nini maoni yako??
12
14
65
RT @ExMayorUbungo: Freeman Aikaeli Mbowe Kwangu umekuwa siyo tu kiongozi wangu wa chama bali ni mwalimu, mwanafalsafa,mkufunzi,mzazi,mlez…
0
455
0
RT @HKigwangalla: Tuhuma za rushwa ni mbaya sana katika tuhuma anazoweza kupewa mwanasiasa. Hususan kama mwanasiasa huyo anajielewa na mais…
0
22
0