mshambuliaji Profile Banner
Maulid Kitenge Profile
Maulid Kitenge

@mshambuliaji

Followers
2M
Following
1K
Statuses
61K

HEAD OF SPORTS WASAFI FM

Joined November 2012
Don't wanna be here? Send us removal request.
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
1 hour
@sucre7548 We unaijua ipi?
2
0
0
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
2 hours
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amempangia Balozi Dkt. Habib Galuss Kambanga kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda. #KitengeUpdates
Tweet media one
2
4
59
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
7 hours
MADUDU YAIBULIWA UJENZI UWANJA WA NDEGE MSALATO
1
0
21
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
7 hours
CHADEMA YATANGAZA MSIMAMO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
0
0
16
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
12 hours
Los Angeles, Calfornia 🇺🇸🇺🇸🇺🇸🇺🇸
Tweet media one
Tweet media two
15
3
161
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
18 hours
SoFi Stadium, Calfornia 🇺🇸🇺🇸🇺🇸
Tweet media one
Tweet media two
Tweet media three
Tweet media four
5
3
65
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
19 hours
Bao la dakika za jioni kutoka kwa James Tarkowski limeinusuru Everton na kipigo kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool katika dimba la Goodison Park kwenye Derby ya Jiji la Liverpool. Liverpool inasalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England pointi 57 baada ya mechi 24 huku Everton imekwea mpaka nafasi ya 15 pointi 27 baada ya mechi 24. FT: Everton 2-2 Liverpool ⚽ 11' Beto ⚽ 90+6' Tarkowski ⚽ 16' Mac Allister ⚽ 73' Salah #KitengeSports
Tweet media one
2
2
145
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
20 hours
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni John Peter (45) Dereva na Mkazi wa Manyire Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na Jafari Shirima (62) Dereva na Mkazi wa Singida kwa kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha Lucy John (40) mkazi wa Manyire. Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo amesema kuwa Katika tukio hilo lililotokea tarehe 12.02.2025 muda wa 08:00 usiku huko maeneo ya Nganana barabara ya Afrika Mashariki mtuhumiwa John Peter aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 499 CRR aina ya Noah aligonga kwa nyuma gari lilokuwa limeegeshwa barabarani lenye namba za usajili T 629 CLB aina ya Scania ikiwa na tela lenye namba za usajili T 447 BSL likiwa na Dereva aitwae Jafari Shirima na kusababisha kifo cha Lucy John ambaye alikuwa abiria katika gari aina ya Toyata Noah. SACP Masejo amefafanua kuwa mara baada ya kugonga gari hilo kwa nyuma mtuhumiwa John Peter alimshambulia Dereva Jafari Shirima na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake. Aidha amebainisha kuwa Majeruhi anaendelea kupatiwa matibabu na mwili wa marehemu umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi wa kitaaalam. Kamanda Masejo akisistiza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa wito kwa kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarabni ili kuepuka ajali. Pia tunatoa wito kwa watu kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi. #KitengeUpdates
Tweet media one
5
9
130
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
20 hours
Aliyekuwa kocha wa Yanga Sc, Sead Ramovic ameshinda mchezo wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Nchini Algeria kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya klabu ya USM Khenchela. Kwa ushindi huo CR Belouizdad imekwea kileleni mwa msimamo wa Ligi ikifikisha pointi 29 baada mechi 16, wakiwa alama moja mbele ya MC Alger waliopo nafasi ya pili huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi. FT: CR Belouizdad 3-0 Khenchela ⚽ 27' Mayo ⚽ 51' Hamroune ⚽ 86' Boukerchaoui #KitengeSports
Tweet media one
13
11
1K
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
21 hours
Ishi Maisha ya kwako✍🏼
Tweet media one
0
1
60
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
1 day
Ndege zote zilizosajiliwa nchini Rwanda au kwingineko lakini zenye Makao yake nchini Rwanda, zimepigwa marufuku kuruka juu ya anga ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mamlaka ya DR Congo imechukua hatua hiyo kutokana na vita vya uchokozi vilivyosababisha vifo vya Wacongo 3,000 ndani ya siku nne huko Goma. Katika robo ya mwisho ya 2024, Rwanda ilivuruga mawimbi ya GPS Mashariki na kuhatarisha abiria wanaoingia kwenye njia za kibiashara katika sehemu hii ya nchi. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ulishutumu tabia hiyo ambayo ni kinyume cha katika sekta hiyo. Itakumbukwa kuwa mnamo Agosti 1998, Wanajeshi wa Rwanda walipanda Ndege ya kiraia ya Congo ili kusafirisha Wanajeshi hadi kambi ya kijeshi ya Kitona (Kongo ya kati, Magharibi mwa nchi) katika jaribio la kuichukua Kinshasa. #KitengeUpdates
Tweet media one
15
22
683
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
1 day
JESHI la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia Watuhumiwa wawili ambao ni Dickson Paul Tamba (27) Mjasiriamali, Mkazi wa Mkuti chini machinjioni Wilaya ya Masasi na Mohamed Ally Kajao (34) Mwalimu Shule ya Msingi Nanyani, Mkazi wa magomeni Wilaya ya Mtwara kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Akitoa taarifa leo Februari 12, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman amesema tukio hilo lilifanyika mwezi Januari 2025 katika nyumba ya kulala Wageni (jina limehifadhiwa). Taarifa ya Polisi imesema wawili hao walikamatwa baada ya Dickson Paul Tamba kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na Mwalimu Mohamed Kajao huku wakijirekodi video kisha kuisambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijami. #KitengeUpdates
Tweet media one
11
5
132
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
1 day
Ukiwa na hasira usifanye maamuzi utaishia kujiumiza mwenyewe✍🏼
Tweet media one
0
2
61
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
1 day
JESHI la Polisi Mkoa wa Lindi limebaini chanzo cha ajali ya basi la Timu ya Mpira wa Miguu ya Dodoma Jiji kutumbukia katika Mto Matandu ambapo limesema dereva wa basi hilo Erasto Nyoni alikuwa kwenye mwendo kasi, pasipo kuchukua tahadhari ya ubovu wa barabara baada ya kuharibiwa na mvua msimu uliopita. Taarifa ya leo Februari 12, 2025 iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Andrew Ngassa imeeleza kuwa baada ya kwenda kukagua eneo la tukio, ambapo amebainisha kuwa basi hilo lilikuwa linatokea Ruangwa na lilikuwa limebeba watu 36 miongoni mwao wachezaji walikuwa 24 pamoja na benchi la ufundi watu 12. "Gari hili lilikuwa linarudi Dodoma kupitia Dar es Salaam lilikuwa limebeba watu 36 miongoni mwao wachezaji walikuwa 24 pamoja na benchi la ufundi watu 12. Lilipofika kwenye daraja la Matandu lilimshinda dereva na kutumbukia katika mto huo, na kusababisha majeruhi ya watu wanane," ——amesema ACP Ngassa. Ajali hiyo ilitokea Frbruari 10, 2025 majira ya saa tatu asubuhi katika Kijiji cha Matandu wilayani Kilwa wakati timu hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka wilayani Ruangwa kwenye mchezo wake na timu ya Namungo FC. #KitengeSports
Tweet media one
90
37
1K
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
1 day
Takribani watu 26 wamekufa katika ajali baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka huko Oromia, Jimbo kubwa zaidi la Ethiopia. Basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Shambu, Magharibi mwa nchi hiyo, kuelekea Mji Mkuu, Addis Ababa. Afisa wa eneo la Wollega Mashariki aliripoti kwamba mbali na waliokufa, watu 43 walijeruhiwa, na idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Hakuna maelezo zaidi yaliyopatikana mara moja. Ajali za barabarani ni tukio la mara kwa mara nchini Ethiopia, ambapo mahitaji ya leseni ya udereva hayazingatiwi, na magari hayatunzwi vizuri. Watu wasiopungua 71 waliuawa mwishoni mwa Desemba mwaka jana katika Jimbo la Kusini mwa Ethiopia la Sidama, wakati lori lililojaa watu lilipoanguka kwenye mikoko. #KitengeUpdates
Tweet media one
Tweet media two
2
0
40
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
1 day
Baada ya kuondoka JS Kabylie Januari iliyopita, kocha wa Algeria Abdelhak Benchikha yuko mbioni kutia saini ya kuifundisha klabu ya Modern Future ya Misri inayoshiriki ligi kuu nchini humo. Benchikha, ambaye tayari amekuwa na uzoefu kadhaa nje ya nchi, hasa Tanzania,Morocco na Qatar, anaweza kujikuta akiwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo. Modern Future FC ni klabu ya soka ya Misri yenye makao yake mjini Cairo ambapo ilianzishwa mwaka 2011,ikiwa ina miaka miaka 14 baada ya kuanzishwa kwake. Klabu hiyo inakamata nafasi ya mwisho Ligi Kuu nchini Misri ikiwa na alama 7 katika michezo 12 iliyocheza. Imeshinda mchezo mmoja tu. #KitengeSports
Tweet media one
4
13
767
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
2 days
Real Madrid imetoka nyuma 2-1 na kushinda 3-2 dhidi ya Manchester City katika dimba la Etihad na kutanguliza mguu mmoja kwenye hatua ya 16 bora ya klabu Bingwa Ulaya. FT: Man City 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 2-3 🇪🇸 Real Madrid ⚽ 19' Haaland ⚽ 80' Haaland (P) ⚽ 60' Mbappé ⚽ 86' Diaz ⚽ 90+2' Bellingham FT: Juventus 🇮🇹 2-1 🇳🇱 PSV FT: Sporting 🇵🇹 0-3 🇩🇪 Dortmund #KitengeSports
Tweet media one
6
5
341
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
2 days
Sio kila Mtu ataona thamani yako✍🏼
Tweet media one
0
3
99
@mshambuliaji
Maulid Kitenge
2 days
TANZIA: Mwimbaji mkongwe wa taarab wa Zanzibar, Bi. Mwapombe Hiyari, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne 11.02.2025. Zama za uhai wake, pamoja na kuimba nyimbo nyingi za taarab, Bi. Mwapombe ameweka alama isiyofutika kwa kuimba wimbo maarufu wa ‘Sabalkheri Mpenzi’ akishirikiana na gwiji mwingine wa taarab wa Zanzibar, Sammi Hadji Dau na baadae Abeid Bakari. #KitengeUpdates
10
12
233