![Othman Masoud Othman Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1725169458887454721/7kjQrQ5f_x96.jpg)
Othman Masoud Othman
@othmasoud
Followers
12K
Following
34
Statuses
539
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa
Zanzibar West, Tanzania
Joined March 2021
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kaka yetu, Ahmed Rajab kilichotokea London jana. Zanzibar tumeondokewa na mmoja wa watu wake walioipenda, kuitangaza na kuipigania kwa dhati kupitia majukwaa tofauti. Tasnia ya Habari imepoteza gwiji na mbobezi. Harakati za kupigania haki duniani zimepoteza mmoja wa wapambanaji shupavu. Mwenyezi Mungu Ailaze roho ya Marehemu mahala pema Peponi.
14
30
166
Leo Januari 27, 2025, nimejumuika na Viongozi, Wananchi, na Waumini mbali mbali wa Kiislamu katika Dua Maalum ya Kuwakumbuka Viongozi Waasisi, Wanaharakati wa Upinzani, na pia Kuwaombea-Dua Wananchi Waliouawa bila ya Hatia, mnamo Januari 26 na 27, Mwaka 2001, Visiwani hapa, iliyofanyika huko Msikiti wa Wakfu wa Mwitani, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
3
27
110
Kwa dhati kabisa nakupongeza ndugu yangu @TunduALissu kwa kuchaguliwa kwako kuwa Mwenyekiti wa @ChademaTz Taifa. Ushindi wako unadhihirisha imani kubwa waliyo nayo wanachama wa chama chako kwako. Nakutakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yako na nina imani kubwa kuwa tutashirikiana katika harakati za kupigania demokrasia hapa nchini na kuwaletea Watanzania mabadiliko wanayoyataka. Hongera sana!
24
200
1K