![Edwin Odemba Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1605249407045275655/tJ_GIoty_x96.jpg)
Edwin Odemba
@chiefodemba
Followers
41K
Following
6K
Statuses
1K
MTANGAZAJI WA TAIFA. Host MEDANI ZA SIASA, Udsm Alumnus, LUO ICON, CEO. CHIEF ODEMBA ENTERPRISES LTD.
Dar es Salaam, Tanzania
Joined September 2017
Tarehe 27/01/2025 M/Kiti wa JUMIKITA Bw Shabani Matwebe alilala polisi kwa zaidi ya masaa 24 huko Rufiji, hata hivyo yeye ameeleza kuwa alilala Polisi kwa sababu ya usalama wake. SHABANI MATWEBE. @chiefodembatz @medanizasiasa
3
8
48
MIMBA ZAIDI YA 200,000 ZAHARIBIKA 2024. SERIKALI imesema kwa mwaka 2024 iliwapokea na kuwapa huduma jumla ya wanawake na wasichana 213, 675 waliopata changamoto ya kuharibika kwa ujauzito nchini. Vilevile, serikali imeliarifu Bunge kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi 2024, wanawake 92 walipoteza maisha kutokana na changamoto mbalimbali zilizosababishwa na kuharibika kwa ujauzito. Hayo yamesemwa Bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Fatuma Toufia, aliyetaka kujua idadi ya wasichana na wanawake walioathirika na utoaji mimba usio salama nchini. Akijibu swali la mbunge huyo, Dk. Mollel alibainisha kuwa kati ya wagonjwa 213,675 waliopatiwa matibabu baada ya ujauzito kuharibika mwaka 2024, wasichana 181, 071 walipatiwa huduma na kuruhusiwa kama wagonjwa wa nje na 32,512 walipatiwa huduma wakiwa wamelazwa. @chiefodemba @medanizasiasa
6
5
33
“UCHAGUZI UMEISHA, DEMOKRASIA UMESHINDA” YERICKO NYERERE. Mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema ndg Yericko Nyerere, amempongeza Tundu Lissu kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa. Yericko ametoa pongezi hizo katika ukurasa wake wa instagram ambapo pia Nyerere amemshukuru Mhe. Mbowe kwa namna ambavyo ameongoza chama hicho kwa muda wote wa uongozi wake. Itakumbukwa kwamba yericko alikuwa mpinzani mkubwa wa Tundu Lissu, na kwa mara kadhaa kupitia vyombo vya habari Yericko aliliambia umma kuwa Tundu Lissu awezi kushinda uchaguzi Duniani hata Mbinguni, lakini pia alisema iwapo Lissu atakuwa mwenyekiti wa chadema, chadema itakufa ndani ya miezi miwili kwani Tundu Lissu hana fedha hata kujisimamia mwenyewe atawezaje kuongoza chama chenye mamilioni ya wanachama..? Aliuliza Yericko. Pamoja na hayo Yericko amesikitishwa na watu wa karibu waliyomsaliti mhe Mbowe, ya kwamba hata walipomwambia Mbowe kuhusu wanaomsaliti bado mheshimiwa Mbowe alisema waache demokrasia ufanye kazi, lakini pia Yericko amekiri timu yake kushindwa katika kinyanganyiro hicho. @chiefodemba @YerickoNyerereT
23
19
157
“WALIOCHAGULIWA WANASTAHILI KUIONGOZA CHADEMA”MMM Mwanaharakati maarufu na kada wa Chadema ndg Martin Maranja Masese amewarai wana Chadema kujikita katika kujenga chama na kupambana na CCM na siyo kulumbana wao kwa wao. Masese ametoa rai hiyo katika ukurasa wake wa X zamani twitter, ambapo amewaasa wanachadema kujivunia namna ambavyo wamewafundisha vyama vingine maana ya demokrasia katika Uchaguzi. “Uchaguzi wetu umemalizika, na sasa tunajenga taasisi yetu. Baada ya uchaguzi mshindi ni CHADEMA. Tujivunie tulivyowafundisha demokrasia wengine” MMM Aidha Bw Masese Viongozi wataondoka, CHADEMA itabaki. Muhimu kuilinda CHADEMA kwa wivu mkubwa. Waliochaguliwa ni wanachama wa CHADEMA. Wanastahili kuongoza. @chiefodemba @medanizasiasa @IAMartin_
#Chiefodembauptades
38
59
603
MSIGWA: MIMI SIMPONGEZI MBOWE. Alieyekuwa Mbunge wa Iringa mjini na Mwenyekiti wa zamani wa kanda ya Nyasa (CHADEMA) kwa sasa kada wa CCM Mch. Peter Msigwa , amesema hampongezi mwenyekiti wa chadema wa zamani mhe. Freeman Mbowe kwa kukubali kushindwa katika uchaguzi ulioisha mapema wiki hii. “Kaka mimi sikupongezi hata kidogo, wanaokupongeza ama wameamua kukufurahisha au ni wale wasiokujua, Wewe uliweka mazingira ya kidemokrasia sio kwa sababu ni mwana demkrasia bali uliamini utashinda kwa kuwa ulidanganywa kuwa unawapiga kura zaidi ya mia sita, ambao waliwekwa sehemu mbalimbali kusafirishwa na kulishwa” Msigwa. Msigwa amesema hayo katika ukurasa wake wa X akikoment katika posti iliyopostiwa na mheshimiwa Mbowe katika ukurasa wake wa X akimpongeza Tundu Lissu kwa ushindi.
93
44
715
Breaking News Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu, amependekeza jina la John Mnyika kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na Baraza kuu la chama limempitisha jina hilo. Wakati huo huo amependekeza jina la Amani Golugwa kuwa naibu katibu mkuu wa chadema Bara, ambaye pia jina lake limepitishwa na Baraza kuu. #Chiefodembaupdates
23
96
954