![Abdulmajid Nsekela Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1855322380849328129/XBFSpm4F_x96.jpg)
Abdulmajid Nsekela
@amnsekela
Followers
14K
Following
297
Statuses
467
Group CEO @CRDBBankPlc | Chairman of @ushirika_tcdc | Former Chairman of @tba_forbankers
Dar es Salaam, Tanzania
Joined December 2019
Umekua wakati mzuri leo kukutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Nicodemus Mkama pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Peter Nalitolela. Mazungumzo yetu yamejikita katika kuboresha mahusiano baina ya taasisi zetu ili kuweza kutoa mchango zaidi katika masoko ya mitaji na dhamana. Sambamba na hilo tumeweza kushiriki katika fainali za Shindano la Utafiti chini ya uratibu wa CFA Society E.A(Chartered Financial Analysts Society East Africa). Shindano hili la kila mwaka linatoa fursa kwa wanafunzi wa vyuo kupata mafunzo ya vitendo katika uchambuzi wa masuala ya fedha ambapo kwa mwaka 2024/25 Benki ya CRDB imechaguliwa kuwa taasisi ambayo shindano hilo litajikita katika kufanyia utafiti. Shindano la mwaka huu litahusisha wanafunzi wa vyuo kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda ambapo mbali na kudhamini shindano hilo, kwa niaba ya Benki yetu nimeahidi kutoa nafasi 5 kwa wanafunzi kutoka Tanzania watakaofanya vizuri kupata ajira. Nimshukuru kaka yangu, CPA Nicodemus Mkama kwa kuahidi kuwa CMSA itawapa mafunzo ya ziada ya vitendo wanafunzi hao watano kabla ya kuajiriwa na Benki yetu.
5
7
38
Nimekua na mazungumzo mazuri na Mhe. Shaib Hassan Kaduara, Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya namna gani Benki yetu na Wizara yake zinaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha sekta ya maji, nishati na madini visiwani Zanzibar. Benki ya CRDB imekua mdau mkubwa wa maendeleo visiwani Zanzibar kupitia mtadao wetu wa matawi katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo mbali na kutoa huduma za fedha, tumekua tukishiriki katika uwezeshaji wa jamii ambapo kwa miaka 5 iliyopita tumewekeza zaidi ya Bilioni 3.5 katika miradi ya kijamii.
1
0
9
Today, I had an opportunity to attend the second day of the Energy Summit at JNICC in Dar Es Salaam, where I had the pleasure of meeting the esteemed Ambassador of Denmark, Mr. Jesper Kammersgaard, along with his dedicated delegates, Mr. Anders Ørnemark and Ms. Karin Poulsen. Our discussions were inspiring and forward-looking, as we explored the immense potential for collaboration between Denmark and Tanzania. I was truly moved by their enthusiasm for seeking opportunities in our beautiful country and connecting with strategic partners. Together, we can pave the way for sustainable energy solutions and foster meaningful partnerships that benefit both nations. 🇹🇿🤝🇩🇰 #EnergySummitinDar #TanzaniaDenmark #SustainableFuture #GlobalPartnerships
6
15
130
It is an honour to participate and engage with different stakeholders in the Africa Head of State Energy Summit in Dar es Salaam. Collaboration in expanding energy access and expediting the continent's clean energy transition is crucial for our collective future. Through concerted efforts, we can achieve sustainable energy solutions for Africa. #EnergySummitinDar
7
10
98
Umekuwa wasaa mwingine mzuri wa kukutana na Balozi wa Tanzania 🇹🇿 nchini Uingereza 🇬🇧, Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki. Tumezungumza mengi ikiwamo ushirikiano wetu na Ubalozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Serikali kwa ujumla kupitia dirisha letu la huduma kwa Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora Banking). Vilevile tumeendelea kujadili juu ya kuwawezesha Diaspora kunufaika na fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo nchini ikiwemo uwekezaji kupitia hatifungani ambao ni uwekezaji wa uhakika na salama kwao. Kupitia kauli mbinu yetu ya "Ulipo Tupo", tunaahidi kuendelea kubuni bidhaa na huduma zitakazosaidia kukuza uchumi wa Taifa letu na watu wetu popote walipo. #ulipotupo
5
5
92
Mapema leo asubuhi nimepata nafasi ya kushiriki mbio zilizoandaliwa na mmoja kati ya wadau wetu wakubwa Tanfoam Arusha @tanfoam. Nawapongeza kwa maandalizi mazuri ya mbio hizi ambazo ni sehemu ya kuhamasisha utaratibu wa kufanya mazoezi kwa jamii yetu ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza. #TanfoamMarathon2024
1
2
38
Nimepata nafasi ya kufika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kumuaga aliekua Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru. Kama ambavyo aliwahi kusema Rais wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, maisha ya binadamu katika ulimwengu huu ni hadithi na kuwa yatupasa kuhakikisha tunaacha hadithi nzuri hapa ulimwenguni. Hakika Lawrence Mafuru ameacha hadithi nzuri katika ulimwengu huu kwa mengi ambayo yameshuhudiwa na wale waliopata nafasi ya kuwa sehemu ya maisha yake. Naendelea kutoa pole kwa familia na ndugu wa marehemu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA libarikiwe🙏🏽
12
17
119
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru. Mbali na kulitumikia Taifa letu katika nyadhifa mbalimbali, Bw. Mafuru atakumbukwa kama kiongozi mwenye maono ambae ametoa mchango mkubwa katika taasisi mbalimbali za fedha hapa nchini ikiwemo Benki yetu ya CRDB akiwa Mjumbe Huru wa Bodi. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA libarikiwe🙏🏽
13
22
266
Our Bank, @CRDBBankPlc, has once again been recognized by Global Finance as the Safest Bank and Best Bank in Tanzania at the 31st Annual Awards Ceremony, held on the sidelines of the IMF and World Bank Annual Meetings in Washington, D.C. This marks our fifth consecutive win for Best Bank and our second for Safest Bank in Tanzania. These awards highlight our commitment to delivering exceptional service, creating value for our stakeholders, and making a positive impact in the financial sector. Thank you to our customers, partners, and dedicated staff for driving CRDB Bank to new heights!
4
4
34
Honored to share insights on digital payments at the World Economic Summit. @CRDBBankPlc has been at the forefront of digital transformation, pioneering platforms that bring banking right to our customers' fingertips. From SimBanking to innovative financial inclusion solutions, we’re creating pathways for a more accessible, inclusive future in Tanzania’s banking sector. Join us in embracing the future of finance! #WES2024
5
9
41
Mama yangu ni baraka kubwa kwangu, mwalimu wangu wa upendo na uvumilivu. Kila siku najifunza kutoka kwako namna ya kuwa na moyo safi na huruma. Amahakika yatupasa kuwaheshimu na kuwajali wazazi wetu kama ilivyoandikwa katika Qur'an: 'Na tumemuamrisha mtu awafanyie wema wazazi wake.' (Surah Luqman, 31:14). Alhamdulillah kwa zawadi ya mama 🫶. #MwanaKijiji#UpendoWaMama
21
31
376
In just a few minutes, I’ll be joining the #WorldEconomySummit2024 panel to discuss how strong payment systems and financial access can drive business growth and empower consumers. Click the link to follow the discussion and join us in exploring the future of digital payments!
3
14
44
Nimeshiriki mkutano wa kusheherekea miaka 30 ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii @esrftz uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi alikua ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, @dr_philip_isdor_mpango. Nawapongeza @esrftz kwa kuadhimisha miaka 30 nikiamini wataendelea kuwa taasisi inayotoa mchango mkubwa katika nchi yetu kupitia tafiti ambazo zitaleta majawabu juu ya changamoto zetu za kiuchumi na kijamii.
5
9
67
Nimeshiriki zoezi la kujiandikisha kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kata ya Msasani. Nikumbushe Watanzania wenzangu kuwa kujiandikisha ni jambo moja lakini muhimu zaidi tujitokeze siku ya kupiga kura kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo katika mitaa yetu na Taifa kwa ujumla.
13
11
151
Nikiwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) nina furaha kubwa kuona mchakato wa kuanzisha Benki ya Ushirika Tanzania (CBT) umekamilika, na leo tumeshuhudia AGM ya kwanza. Shukrani za dhati kwa Mhe. Rais, Dkt. @SuluhuSamia Mhe. Waziri @HusseinBashe na wadau wote kwa mchango wao. Mafanikio haya ni hatua kubwa katika kuimarisha sekta ya ushirika nchini. #AGM #CBT #UshirikaImara
10
24
116
Nimepata heshima kubwa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti na Rais wa MasterCard, Jon Huntsman kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa #UNGA79 unaofanyika New York, US. Tumezungumza mengi ikiwamo utekelezaji wa Mpango wa Uwezeshaji Wakulima nchini Kidijitali wa 'MADE Alliance Africa 🌍 .' Nikiwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ushirika (TCDC) ninaamini mpango huu utakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwa wakulima wetu nchini zaidi ya milioni 8 kwa kuboresha kilimo chao kupitia teknolojia za kisasa na huduma za fedha kidijitali. Serikali kupitia TCDC ilishaanza mchakato wa uanzishwaji wa mfumo wa kidijitali kama sehemu ya kuimarisha ushirika nchini. Hivyo mpango huu wa MADE Alliance Africa unakuja kuchochea jitihada hizi na kuleta tija zaidi kwa wakulima wetu.
15
32
157
Our Bank's delegation, led by Vice Chair of Board, Prof. Neema Mori, met with Citibank @Citi leadership on the sidelines of UNGA 79. The discussion focused on strengthening our partnership, especially in facilitating trade, and collaboration on CRDB Bank’s expansion into new markets, including EAC and SADC. As the only Tanzanian Bank operating across borders in Burundi and DRC, such a partnership is vital for enhancing our regional operations and footprint, boosting our trade financing efforts, and delivering greater value to our customers and stakeholders.
4
10
63
Leo nimepata heshima ya kushiriki ibada na kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la mtaa wa Katembe Usharika wa Kituntu. Usharika huu upo chini ya Kanisa la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe chini ya uongozi Baba Askofu Dkt. Benson Bagonza. Mungu amekua mwema kwetu kwa kutuwezesha kufanikisha harambee hii kwa mafanikio makubwa sana. Kipekee sana nimshukuru Baba Askofu Dkt. Bagonza na uongozi wote wa Dayosisi kwa kunipa heshima kubwa ya kuongoza harambee hii muhimu kwa ujenzi wa Usharika wa Kituntu. Kama ambavyo neno la Mungu kutoka 2 Wakorintho 9:7 linavyosema "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu", Mungu awabariki wote tulioshirikiana katika baraka hii na kujitoa kwa moyo mkunjufu.
14
19
188