WiLDAF Tanzania
@WiLDAFTz
Followers
11K
Following
7K
Statuses
8K
WiLDAF- Tanzania is a Pan Africa Network Organization, Strategically linking Law and Development for the betterment of Women's lives. Free Legal Aid 0800780070
Dar es Salaam, Tanzania
Joined November 2014
WiLDAF Tanzania tumeshiriki uzinduzi wa One Stop Center Tarime, Mkoa wa Mara, kituo kilichojengwa kupitia mradi wa Chaguo Langu, Haki Yangu unaofadhiliwa na Ubalozi wa Finland na kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya WiLDAF Tanzania na UNFPA. Kituo hiki kitakuwa kikitoa huduma jumuishi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ikijumuisha huduma za ustawi wa jamii, Afya ya mwili na akili, Polisi pamoja na chumba maalum cha kuhudumia watoto. Mgeni rasmi wa tukio hili alikuwa Mh @gwajimad , akiambatana na Balozi wa Finland nchini Tanzania, H.E Theresa Zitting, na Mwakilishi wa UNFPA Tanzania, Mark Bryan. Uzinduzi huu pia ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Maendeleo na mashirika mengine ya haki za binadamu. Mabinti walionufaika na mradi pamoja na wazazi wao walishiriki tukio hili na kushuhudia jinsi mradi ulivyobadili maisha yao. #ChaguoLanguHakiYangu #OneStopCenterTarime #wildaftz
0
3
6
RT @UNFPATanzania: 📍Happening Now in Tarime, #Mara Region 🇹🇿! *Chaguo Langu, Haki Yangu / My Rights, My Choice* program Hon. Minister @…
0
15
0
RT @UNFPATanzania: 📌“For Finland 🇫🇮 , the rights of women & girls, inclusiveness, & non-discrimination are at the core of our Foreign Polic…
0
5
0
RT @Dr_DGwajima: 8 Februari, 2025 kazi inaendelea mchana huu..... Picha hizi ni baada ya uzinduzi wa kituo jumuishi cha huduma kwa manusur…
0
10
0
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji – Mkoa wa Mara @wildaftz kwa kushirikiana na mashirika mengine wakiwemo @unfpatanzania @Atfgm_Massanga, C-Sema,Tanzaniainterfaithpartnership na @helpagetanzania tumeungana kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji – Mkoa wa Mara. Maadhimisho haya yamehudhuriwa na Serikali ya Mkoa wa Mara, Jeshi la Polisi, wananchi kwa ujumla, pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali. Washiriki walijitokeza kwa wingi wakibeba jumbe zenye kuhamasisha jamii kuachana na ukeketaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ukatili huu kwa wasichana na wanawake. #TokomezaUkeketaji
0
0
1
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji – Mkoa wa Mara @wildaftz kwa kushirikiana na mashirika mengine wakiwemo @unfpatanzania @Atfgm_Massanga, C-Sema,Tanzaniainterfaithpartnership na @helpagetanzania tumeungana kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji – Mkoa wa Mara. Maadhimisho haya yamehudhuriwa na Serikali ya Mkoa wa Mara, Jeshi la Polisi, wananchi kwa ujumla, pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali. Washiriki walijitokeza kwa wingi wakibeba jumbe zenye kuhamasisha jamii kuachana na ukeketaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ukatili huu kwa wasichana na wanawake. #TokomezaUkeketaji
0
0
1
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji – Mkoa wa Mara @wildaftz kwa kushirikiana na mashirika mengine wakiwemo @unfpatanzania @Atfgm_Massanga, C-Sema,tanzaniainterfaithpartnership na @helpagetanzania tumeungana kuadhimisha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukeketaji – Mkoa wa Mara. Maadhimisho haya yamehudhuriwa na Serikali ya Mkoa wa Mara, Jeshi la Polisi, wananchi kwa ujumla, pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali. Washiriki walijitokeza kwa wingi wakibeba jumbe zenye kuhamasisha jamii kuachana na ukeketaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ukatili huu kwa wasichana na wanawake. #TokomezaUkeketaji
0
0
2
@wildaftz kupitia mradi wetu wa chaguo langu haki yangu unaofadhiliwa na Ubalozi wa @finlandintanzania na kutekelezwa na @wildaftz na @unfpatanzania, tumekuwa tukitoa elimu ya kupinga ukeketaji katika wilaya ya Butiama, Serengeti na Tarime, Pia Katika jitihada hizi tumefanikiwa kuokoa mabinti waliokusudiwa kukeketwa na kuwapeleka kwenye nyumba salama. Sambamba na jitihada hizi tumekua tukiandaa sherehe mbadala za kuwavusha rika watoto wa kike bila kukeketwa ili wasijione kuwa sio sehemu ya jamii. Ni jukumu letu kuhamasisha jamii kuacha mila hii kandamizi ili watoto wa kike waepuke madhara ya ukeketaji na waweze kutimiza ndoto zao. #TokomezaUkeketaji #LindamstotoWakike #WiLDAF #EndFGM
0
1
3
@wildaftz kupitia mradi wa Irish Aid Wanawake Sasa tumeendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwenye makundi mbalimbali ya kijamii ,ikiwemo nyumba za ibada ili kila mtanzania aweze kupata fursa ya kutekeleza haki yake ya msingi ya kushiriki katika michakato ya Kidemokrasia bila kujali jinsia wala itikadi. Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura linaendelea , usiache kushiriki na kuwahamasisha wengine kushiriki zoezi hili la muhimu. #wanawakesasa #irishaidwanawakesasa.
0
0
0
Save the Date!! Join us at the 69th Commission on the Status of Women (CSW69) for an engaging side event hosted by WiLDAF Tanzania: Theme:“Generation Equality Towards Beijing +30: Addressing Rural Women’s Land Tenure Insecurity and Gender Inequality.” Date: 13rd March 2025 Time: 03:00 PM – 04:15PM Room:CR-E This powerful session will highlight best practices, success stories, and innovative strategies to amplify women’s land rights, combat gender-based violence, and empower women. Featuring insights from WiLDAF Tanzania, Landesa and Stand For Her Land Tanzania, this event underscores the importance of multistakeholder partnerships in advancing gender equality and economic empowerment. #CSW69 #Beijing+30 #GenerationEquality #WomenLandRigh #S4HL #wildaftz
0
1
2
@wildaftz ikiwakilishwa na Mratibu wa Kitaifa, Wakili @annakulaya tulishiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtakatifu Brigid yaliyoandaliwa na @IrlEmbTanzania kwa uongozi wa @IEAmbDar Mhe. Nicola Brennan, Balozi wa Ireland nchini Tanzania na kuhudhuriwa na Mhe. Frances Fitzgerald, aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Haki na Usawa wa Ireland, kama Mgeni Maalum na Mzungumzaji Mkuu. Maadhimisho haya yanafanyika kwa heshima ya Mtakatifu Brigid, mmoja wa Watakatifu Wakuu wa Ireland, anayejulikana kwa mchango wake katika elimu, haki za wanawake, na uongozi . kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kuimarisha Ushiriki wa Wanawake Katika Siasa – Uzoefu wa Ireland na Tanzania Katika Kuvunja Vikwazo," Tunashukuru Ubalozi wa Ireland kuendeleza ushirikiano wa kudumu katika kuimarisha usawa wa kijinsia na ushiriki wa wanawake katika siasa. #Wanawakesasa
0
2
5
Jiandikishe sasa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, zoezi hili linaendelea kwa mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma ( Madaba,Namtumbo na Tunduru) kuanzia tarehe 28 Januari -3 Februari,2025 #wanawakesasa
0
1
1
Je unahitaji huduma ya msaada wa kisheria na unashindwa kwenda kuifuata?. Usijali hata katika kipindi hiki ambapo barabara zimefungwa sisi tumejiandaa kukuhudumia Bure, Cha kufanya ni kupiga simu kwenye namba yetu kama inavyoonekana na tutakupatia huduma Buree. #wildaftz
0
1
0
Je umejiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura? Endelea kufuatilia kurasa zetu ili upate ratiba kamili ya zoezi hili kwa mkoa wako na wilaya yako. #wanawakesasa #womeninleadership
0
1
1
Katika kuadhimisha wiki ya sheria @wildaftz tumeungana na mahakama kuu kanda ya dar es salaam kutoa huduma za msaada wa kisheria bure. Karibu katika banda letu kwenye viwanja vya mnazi mmoja tukuhudumie bure ,Tupo kuhakikisha unapata msaada wa kisheria unaohitaji hata wakati wa changamoto za kufungwa kwa barabara jijini Dar es Salaam.
0
3
5
WiLDAF Tanzania inashiriki kikamilifu Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 25 Januari mpaka tarehe 2 February ,2025. Maonesho ya mwaka huu yanakwenda na kauli mbiu isemayo ;Tanzania ya 2050:Nafasi ya taasisi zinazosimamia Haki madai katika kufikia Malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo. Aidha @wildaftz Tunayo furaha kuwakaribisha kwenye banda letu la msaada wa kisheria, ambapo tunatoa huduma za msaada wa kisheria bure na wanasheria wetu wabobezi watakuwepo kuwahudumia. Karibuni sana
0
1
2
Leo, katika Siku ya Kimataifa ya Elimu, WiLDAF Tanzania tunaendelea kuazimisha dhamira yetu ya kuendeleza upatikanaji wa elimu bora na jumuishi kwa wote, hususan kwa wanawake na wasichana. Elimu ni nyenzo ya kuvunja vizuizi na kuleta ukombozi katika ulimwengu huu wa kiteknolojia. Kupitia program zetu tunaendelea kuwawezesha wanawake na wasichana kwa maarifa, ujuzi, na fursa za kuongoza na kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao. WiLDAF pia inasimama kidete katika kutetea mazingira salama na rafiki kwa wasichana kupata elimu bora bila hofu ya ukatili, ubaguzi, au mila hatarishi. #wildaftz
0
4
8