![Paul Bonaventure Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1612911317446172673/sm0ELxTN_x96.jpg)
Paul Bonaventure
@Phbhimself
Followers
43K
Following
25K
Statuses
35K
|| PEACE MAKER ✌🏿 || Author | - Medicines are my tools!💊 | Pharmacist | A human. Being. | Meditation Instructor 🧘♀️| HipHop🎶 |
Somewhere in Africa
Joined January 2015
Watu wengi wamekuwa wakijifunza meditation tangu karne na karne, miaka na miaka. Sio kitendo kilichoanza hivi sasa bali ni kitendo kilichoanza tangu zamani na kimekuwa na faida mbalimbali kwa watu waliojifunza na kufanya taamuli. Wengine ni kutokana na kupunguza stress, kujifunza kuongoza akili zao, kuachana na mazoea wanayoshindwa kuyaacha na kutokana na kuongeza hekima ya kiimani. Ningependa kuelezea faida chache nzuri ambazo zinapatikana pale mtu anapofanya taamuli vyema na kwa mara kwa mara. • Taamuli (Meditation) inasaidia kutengeneza furaha ya ndani. Tunaposema furaha ya ndani tunamaanisha nini? Ni furaha unayotembea nayo wakati wote. Ni furaha isiyotegemea maisha yako yapoje, ni furaha isiyotegemea una vitu gani bali ni furaha inayopatikana ndani mwako. Wengi hupata furaha kutokana na hali na vitu, na kipindi cha wakati mgumu wao hukosa furaha kwani furaha yao inategemea vitu vya nje ambavyo havidumu milele. Lakini katika meditation unajifunza kuachana na kujishikilia na mawazo, fikra, hisia, na milango ya ufahamu. Unajifunza kuingia ndani na kutafuta kisicho na mwanzo wala mwisho. Ambacho wakati wowote upo nacho, nacho kinakuunganisha source/chanzo na ufahamu mkuu wa Ulimwengu ambao wakati wote mpo pamoja.
2
5
54
@kahumbyanancy @GabrielMunyaga Mimi huwa siandiki kwaajili ya mtu asikie kile anapenda, huwa sichagui upande kwa maana sitaki kupotoka. Napoandika ukaona napingana mtazamo wako njoo na hoja tu, utajibiwa. Asante.
1
0
1