![COSTECH Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/2149468222/costech_tanzania_x96.jpg)
COSTECH
@costechTANZANIA
Followers
13K
Following
143
Statuses
3K
| Official Account of Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) | Get update of whatβs Happening in Tanzania in Research,Technology & Innovation|
Dar es Salaam, Kijitonyama
Joined April 2012
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), UNDP Tanzania (@undptz ) na VodaCom Tanzania (@VodacomTanzania ) wamezindua mashirikiano ya kuandaa wiki ya Ubunifu 2025. Wiki ya Ubunifu 2025 inatarajia kufanyika tarehe 12 mpaka 16 Mei, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam. #InnovationWeek2025 #IWTz2025
0
1
3
RT @IWTZ_: Dr. Athman Mgumia, Director @costechTANZANIA , called for a focus on solutions that matter, collaborations that drive real changβ¦
0
5
0
RT @Said_Hozza: Kicking-Off our Electronics Session at #KibahaBoysSchool Proud Sponsored by @TMEeducation x @taifatek
0
6
0
Uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu (@nungujr ) akitoa ufafanuzi mbele ya Wageni waliotembelea Banda la COSTECH, Siku moja kabla ya Uzinduzi rasmi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023. Tukio hilo linafanyika leo Tarehe 1 Februari 2025, Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre - Jijini Dodoma.
0
3
6
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamesaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa mwaka mmoja unaolenga kukuza Teknolojia na Ubunifu zinazochangia maendeleo ya sekta ya kilimo, usalama wa chakula na ustawi wa jamii nchini Tanzania, tarehe 21 Januari, 2025 katika ukumbi wa COSTECH. Mkataba huo ni muendelezo wa Makubaliano yaliosainiwa baina ya COSTECH na @WFP_Tanzania tarehe 11 Juni, 2024 kwa lengo la kuendeleza Bunifu za kilimo na chakula nchini.
0
5
18
COSTECH yachangia kuleta Mageuzi ya kiuchumi katika Elimu ya juu. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, amesema taasisi za COSTECH, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) zinajukumu muhimu la kusaidia kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia sekta ya elimu ya juu chini ya mradi wa HEET. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kabla ya ruzuku kwa wabunifu ya siku tatu yaliyoanza tarehe 15 hadi 17 Januari, 2025 katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Nungu alieleza kuwa utekelezaji wa jukumu hilo utapimwa kwa mafanikio ya COSTECH katika kushiriki mageuzi hayo. Dkt. Nungu alisisitiza umuhimu wa uwajibikaji miongoni mwa wadau ili kuhakikisha malengo ya mradi wa HEET yanafikiwa. Alieleza pia kuwa vituo vya ubunifu vinapaswa kupewa kipaumbele, kwani vina mchango mkubwa katika maendeleo ya wabunifu na uchumi wa taifa. Kuhusu hali ya kumbi za bunifu katika vyuo vya elimu ya juu, aliahidi kuhakikisha taarifa za mrejesho ya "due diligence" kwa taasisi tano za elimu ya juu zinawafikia viongozi husika ili zifanyiwe kazi kwa uzito unaostahili. Aidha, Dkt. Nungu aliwahimiza washiriki kutumia fursa ya mfuko wa kukopesha wabunifu kwa riba nafuu " Samia Innovation Fund", ambao ulizinduliwa rasmi Desemba 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, kwa lengo la kusaidia wabunifu kubiasharisha bunifu zao.
0
3
7
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu,Disemba 31,2024 amefanya ziara ya kutembelea Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT). Katika ziara hiyo, Dkt. Nungu amepata fursa ya kutembelea ujenzi wa majengo yanayoendelea katika Mradi wa Mageuzi ya Elimu ya Juu (HEET).
0
2
11
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu [@nungujr ] amepata fursa ya kushiriki katika wiki ya Kampuni changa (Startups) Tanzania. Tukio hili limewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, wawekezaji, viongozi na watunga sera kujadili fursa na changamoto za kampuni changa duniani. Aidha Mkurugenzi wa COSTECH Dkt. Amos Nungu alipata fursa ya kuzungumzia mambo yanayofanywa na COSTECH kama vile jukumu la mfuko wa kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MTUSATE) namna unavyosaidia ubiasharishaji wa utafiti na ubunifu. Pia Dkt. Nungu aliezea namna gani mfuko wa dhamana wa kuwezesha kusaidia kukopesha kampuni changa, Kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kukuza mfumo wa ikolojia wa kampuni changa Tanzania. #StartupWeek #TSA
0
3
10
Miradi Mitatu Bora Yatinga Kileleni Programu ya Kuza FemTech Katika hafla ya hitimisho ya Programu ya Kuza FemTech iliyoandaliwa na COSTECH kwa kushirikiana na @UNICEFTanzania kupitia mpango wa BUNI Divaz kutoka @bunihub ambayo ilifanyika Ijumaa ya tarehe 13 Novemba, 2024, miradi mitatu ya kibunifu iliibuka kidedea kati ya saba iliyowasilishwa. Programu hiyo ililenga kuwawezesha mabinti walioko nje ya mfumo rasmi wa shule kwa kuwapatia ujuzi wa ubunifu na kuwahamasisha kujiajiri. Miradi iliyoshinda ni Adorable Candles, BEST CONTENT STUDIO, na Smart Edu 3D, kila mmoja ukionesha mchango wa kipekee katika kuboresha maisha ya jamii. Adorable Candles ni mradi unaojikita katika utengenezaji wa mishumaa ya kisasa yenye harufu nzuri isiyo na madhara na yenye kemikali maalum inayozuia moshi. Ubunifu wa kipekee wa mishumaa tiba yenye dawa ya mbu umelenga kupambana na malaria, hususan katika maeneo ya joto kama Dar es Salaam ambako matumizi ya vyandarua yamepungua. Mishumaa hii inatoa suluhisho la ubunifu si tu kwa afya bali pia kwa urembo, ikilenga wateja wa majumbani, makanisa, hoteli, na ofisi za serikali. Best Content Studio ni mradi unatoa suluhisho kwa changamoto ya upungufu wa mandhari za kisasa kwa matangazo na maudhui ya taasisi za kiserikali, zisizo za kiserikali, na kwa podcasters. BEST CONTENT STUDIO inalenga kuunda studio za hali ya juu zenye mandhari maalum kulingana na mahitaji ya wateja, huku zikiwa na vifaa vya kisasa vya kurekodi sauti na video. Ubunifu wao unajumuisha matumizi ya teknolojia ya kisasa kama VR na AR, na huduma zao zinapatikana kupitia programu tumizi maalum kwa urahisi wa wateja. Smart Edu 3D ni mradi unaotumia teknolojia ya uchapishaji wa 3D kutengeneza vifaa vya kujifunzia, hasa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kama vipofu na viziwi. Vifaa hivi vinatengenezwa kwa plastiki rafiki kwa mazingira (PLA) na vinajumuisha herufi, namba, na maumbo yenye nukta nundu, kuhakikisha urahisi wa kujifunza kwa vipofu. Lengo la mradi huu ni kufikia wanafunzi milioni 3 wa Tanzania kwa muda mfupi na kupanua huduma hadi duniani kote kwa muda mrefu. Miradi hii mitatu bora ilivuta hisia kwa kuonyesha uwezo mkubwa wa kutumia teknolojia na ubunifu kuboresha maisha ya jamii.
0
3
9
RT @TanzaniaSA: We are excited to announce Hon. @JerrySilaa as the keynote speaker for @TZStartupWeek 2024. Register for a long week eveβ¦
0
16
0
Heartfelt gratitude for sponsoring #STICE2024! Your support is a cornerstone of Science,Technology, Innovation and collaboration as we drive forward towards a brighter, tech-powered future. Thank you for believing in the vision! @WBTanzania @vetatanzania @CRDBBankPlc @tanzaniaportshq @Funguo_Tz @eGA_Tanzania @UNICEFTanzania @WIPO @UNCDF @TTCLCorporation
#Gratitude #Partnerships
0
5
13
RT @Funguo_Tz: And that's a wrap! The 9th Annual STICE (Science, Technology, and Innovation Conference and Exhibitions) in Tanzania was anβ¦
0
1
0
RT @TanzaniaSA: π
π«π¨π¦ ππππ‘ - ππππ‘ πππππ¦πππ«, ππ₯π₯ π«π¨πππ¬ π°π’π₯π₯ π₯πππ ππ¨ ππ‘π ππ§π’π―ππ«π¬π’ππ² π¨π πππ« ππ¬ πππ₯πππ¦ (ππππ), πππ° ππ’ππ«ππ«π² ππ¨π« ππ‘π πππ§π³ππ§π’π ππππ«β¦
0
6
0
COSTECH YAWATAKA WAHITIMU WA DIT KUNUFAIKA NA MFUKO WA UBUNIFU Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu (@nungujr ) amewahimiza wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) waliobuni bidhaa zenye uwezo wa kushindana sokoni kutumia Mfuko wa Ubunifu wenye thamani ya TZS bilioni 2.3 ili kuendeleza miradi yao ya kibunifu. Wito huu umetolewa wakati wa Mahafali ya Kumi na Nane ya DIT yaliyofanyika Ijumaa, Desemba 6, 2024. Mfuko huo wa Ubunifu ulizinduliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Tisa la Wanasayansi, Watafiti, na Wabunifu (#STICE2024), lililofanyika Desemba 2 hadi 4, 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Mkurugenzi wa COSTECH alibainisha kuwa Mfuko wa Ubunifu unalenga kusaidia wabunifu na watafiti kwa kuwapatia rasilimali zinazohitajika kuboresha miradi yao na kuhakikisha inafikia viwango vya ushindani wa kimataifa. Aliongeza kuwa ni muhimu kwa wahitimu wa DIT kutumia fursa hii ili kuongeza mchango wao katika maendeleo ya kiteknolojia na kiuchumi nchini. "Wahitimu hawa wameonyesha uwezo mkubwa wa kibunifu, na kupitia Mfuko wa Ubunifu, tunaamini wanaweza kuleta mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na teknolojia, nishati, na viwanda, kilimo na mazingira," alisema. Katika mahafali hayo, wahitimu walihamasishwa kuzingatia maadili, kujifunza zaidi, na kutumia maarifa waliyojipatia DIT ili kuimarisha uchumi wa Taifa kupitia Ubunifu na Teknolojia. #COSTECHTanzania #COSTECH2024
1
8
26
Dar es Salaam, Desemba 4, 2024. Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesisitiza dhamira ya serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu (STU) ili kuwawezesha vijana wa Kitanzania kuona sekta hiyo kama fursa ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Akihitimisha Kongamano la Tisa la Wanasayansi, Watafiti, na Wabunifu (#STICE2024) lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Prof. Mkenda alisema, "Serikali imeahidi kuendelea kuwekeza kwenye STU ili vijana wa Kitanzania waone kuwa sayansi ni fursa na wakimbilie huko na wachangie kusaidia maendeleo yao na ya taifa." Prof. Mkenda pia aliwataka wabunifu kuhakikisha kazi zao zinafika sokoni na kutatua changamoto za kijamii badala ya kurudia bunifu zilezile kila mwaka. "Tunataka kuona kazi za wabunifu zinafika sokoni na kutatua changamoto za jamii, na sio kila mwaka tunaona bunifu hizohizo. Ndiyo maana tumeanzisha Mfuko wa Samia ili mtaji isiwe sababu ya kukwamisha maendeleo," alieleza. Mfuko wa Samia, ambao umetangazwa rasmi, unalenga kusaidia wabunifu na wajasiriamali wa Tanzania kwa kuwapatia mtaji ili kuendeleza bunifu zao na kuzifanya ziweze kusaidia katika kuboresha maisha ya jamii na kukuza uchumi wa nchi. Kongamano hilo la siku tatu, lenye kaulimbiu "Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa Ustahimilivu wa tabianchi na Uchumi Shindani." limekuwa jukwaa muhimu kwa wataalamu wa sayansi, watafiti, na wabunifu kubadilishana mawazo na kutafuta suluhisho za changamoto zinazokumba jamii. Katika hotuba yake ya kufunga, Prof. Mkenda aliwasihi washiriki kutumia maarifa waliyopata katika kongamano hilo kwa vitendo. "Tunayo dhamana ya kuhakikisha kwamba sayansi na ubunifu havibaki tu kwenye maabara bali vinasaidia kubadilisha maisha ya Watanzania," alisema. Wito wa Prof. Mkenda umeongeza matumaini miongoni mwa watafiti,wabunifu, na wadau wa maendeleo, huku serikali ikitarajiwa kutoa msukumo zaidi katika kuhakikisha sayansi inakuwa mhimili wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. #STICE2024 #MamaYupoKazini #Tanzanialnnovation
0
4
7