![Official Bavicha Taifa Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1877998012049379328/iZyWG1SM_x96.jpg)
Official Bavicha Taifa
@bavicha_taifa
Followers
141K
Following
583
Statuses
11K
Zoezi la kuhesabu kura limeanza kwa Baraza la Wazee wa Chadema. #StrongerTogether
#MkutanoMkuuChadema2025
9
6
57
#Ufafanuzi Si kweli kuwa kuna mazingira ya rushwa. Idrissa Kassim alikabidhiwa fedha za nauli kwa wajumbe wa Bavicha kutoka Kanda ya Magharibi, wakati akiwalipa ndio ilitafsiriwa kuwa anatoa rushwa.
85
17
95
Nguvu ya umma imeshinda, Elia Mbise yupo huru.
Elia A. Mbise (20) mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Mwanza amehukumiwa miaka 3 au faini ya milioni 7 kwa kosa la uchochezi. Sasa yupo Gereza la Magu. Tuungane kumchangia faini Tuma mchango wako kwenda 1. Namba 0746 066 518 2. Jina BAVICHA MKOA MWANZA
2
7
56
"Ni muda wa kuchukua hatua. Jiandikishe tuwamwage! Hii siyo tu kauli mbiu, ni mwito wa mabadiliko ya kweli. Umoja wetu utaleta mabadiliko. Sauti zetu zitabadilisha taifa hili. Tupambane, tusikate tamaa, na zaidi ya yote, jiandikishe tuwamwage." Mhe. @John_Pambalu
0
6
20
"Tumeweka mawakala katika vituo kuangalia na kusimamia zoezi la uandikishaji wa wapiga kura." Mhe. @John_Pambalu
0
6
31
"Maendeleo hayaji kwa ahadi tupu. Maendeleo yanahitaji mipango, viongozi waadilifu, na vijana wanaosimama imara. Tusiwe sehemu ya tatizo, tuwe sehemu ya suluhisho. Jiandikishe tuwamwage! Ni muhimu zaidi sasa, kuliko wakati wowote ule, tujitokeze kwa wingi." Mhe. @John_Pambalu
0
4
26
"Tukikosa kujiandikisha, tutakosa nafasi ya kuamua hatma yetu. Tumeona athari za kukaa kimya na kutoridhika na hali ilivyo. Huu si wakati wa kuogopa, huu ni wakati wa kutenda. Jiandikishe tuwamwage." Mhe. @John_Pambalu
0
0
7
"Vijana wengi wameachwa nyuma kimaendeleo. Tunakabiliwa na ukosefu wa ajira, huduma duni za afya, elimu yenye viwango vya chini, na mazingira magumu ya kujiajiri. Serikali imekuwa ikitupatia ahadi tupu, bila utekelezaji wa vitendo. Hatuwezi kusubiri tena." Mhe. @John_Pambalu
0
5
20
"#WatakaWasitake; mitaa, vijiji na vitongoji mwaka huu 2024 vitaongozwa na Chadema. Kufanikisha hilo kila kona ya nchi yetu uelekeo ni Kwenda kwenye vituo vya uandikishaji, tukajiandikishe." Mhe. @John_Pambalu
0
1
5
"Vijana wenzetu ambao mmejiajiri kwenye bodaboda, wamachinga, wananfunzi wa vyuo na vyuo vikuu, wavuvi na makundi mbalimbali ya vijana nawasihi tuchukue muda wa dakika 10 tu Kwenda kujiandikisha kisha tuendelee na zoezi la ujenzi wa taifa letu." Mhe. @John_Pambalu
1
15
35
"Tukihitaji kushinda lazima tuandae wapiga kura, sasa ni wakati wa kuandaa wapiga kura, kisha Novemba Mosi 2024 tukachukue fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika mitaa, vijiji na vitongoji." Mhe. @John_Pambalu
0
9
49
"Leo ikiwa ni siku ya kwanza, hii ni fursa muhimu kwa kila kijana, fursa ya kujitengenezea nafasi ya kuchagua viongozi wa mitaa na vijiji, viongozi watakaosimamia maslahi yetu na kutetea haki zetu." Mhe. @John_Pambalu
0
7
31