![Habari Digital Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1763861684022607872/997YIChT_x96.jpg)
Habari Digital
@HabariDigital_
Followers
229K
Following
277K
Statuses
179K
Kwa Habari, Burudani na Matukio, Kitaifa na Kimataifa, Saa Ishirini na Nne, Siku Saba za Wiki.
Joined May 2020
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa waislamu nchini kuendelea kumcha Mungu na kutenga muda wa kujifunza na kuisoma Qur’aan Tukufu ambayo itawafunza mambo mema yaliyoelekezwa na Mwenyezi Mungu. Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 9, 2025 jijini Dar es salaam wakati akizindua Mashindano Makubwa zaidi ya Qur’aan Tukufu Ulimwenguni 2025. “ Nawaomba msivunjike moyo akitokea mwenye tafsiri tofauti nyie msivunjike moyo wala kukatishwa tamaa bali mfanye mashindano haya yawe kinara na kuutangaza uislamu katika ulimwengu,” amesema Dkt. Biteko. Pia amewahimiza kumuomba Mungu ili Qur’aan iwanyanyue na isiwabwage katika shughuli mbalimbali wanazofanya kama kaulimbiu ya mwaka huu inavyosema “ Qur’aan Ikunyanyue, Isikubwage”. Amesema Qur'aan inatoa funzo kwa watu na kuwa waasisi wake waliyaanzisha kwa ngazi ya madrasa lakini baadaye kutokana na umuhimu wake yakavutia wengi zaidi na kuwa mashindano ngazi ya mtaa, kata, wilaya, mkoa hadi kuwa ya Afrika Mashariki, Bara la Afrika na kisha kufikia ngazi ya kuwa mashindano ya Ulimwengu “ Mashindano haya mbali na kuwa yanachochea usomaji wa Qur’aan Tukufu na hivyo kujenga uelewa wa hofu ya Mwenyezi Mungu lakini pia yanaitangaza Tanzania katika taswira chanya,” amebainisha Dkt. Biteko. Ameendelea kusema kuwa Nabii Musa aliwalingania watu wake kwa kutumia muongozo kutoka katika Taurati, Nabii Daudi yeye akatumia Zaburi, Nabii Issa (Yesu) akatumia Injili na Mtume Muhamad swalla llahu alayhi wasallam akatumia Qur’aan tukufu kuwalingania watu wa umma wake. "Kimsingi vitabu hivi vya muongozo vinamfundisha binadamu tabia njema na kumsihi kuzishikilia na kumuonesha tabia zisizofaa na kumuasa kukaa mbali nazo.” Dkt. Biteko amerejea aya katika Qur’aan tukufu sura ya 35, Surat Faatir, aya ya 28 “… kwa hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni”. Amefafanua “ Aya hii ina maanisha kuwa wale waliopata ujuzi na mafundisho ya Mwenyezi Mungu ambayo yanapatikana katika Qur’aan tukufu na kuyazingatia yale waliyojifunza ndio wanaofika daraja la uchamungu.” Vilevile, Dkt. Biteko ameipongeza Taasisi ya Al- Hikma kwa jitihada zake za kukuza Mashindano ya kuhifadhi Qur’aan Tukufu ulimwenguni. Mkurugenzi Mkuu wa Al- Hikma na Mwenyekiti wa Mashindano ya Qur’aan Tukufu Ulimwenguni, Sheikh Nurdin Kishk amesema kuwa mashindano hayo yameendelea kukua kila mwaka kutokana na mapenzi ya kuhifadhi Qur’aan. Aidha, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wake na kwa kuridhia mashindano hayo kufanyika katika Uwanja wa Taifa mnamo Machi 16, 2025 ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. “ Mashindano haya yanayofanywa na Al- Hikma Foundation yameweka alama ambayo haitafutika na mataifa mbalimbali yameanza kuyaiga. Pia, Mashindano Makubwa Zaidi ya Qur’aan Tukufu Afrika sasa yatajulikana kama Mashindano Makubwa Zaidi ya Qur’aan Tukufu kwa Mabara yote ya Ulimwengu ,” amesema Sheikh Kishk Akizungumza kwa niaba ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ali Ngerukwa amesema kuwa Mufti Mkuu yupo tayari kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo ya Ali- Hikma katika kutekeleza shughuli zao.
2
0
48
VIDEO: Jukwaa la asasi za kiraia linaloundwa na taasisi kutoka nchi kumi na mbili za Afrika, wametoa tamko kufuatia mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jana Februari 8, 2025 Jijini Dar es Salaam, kujadili hatima ya mgogoro ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Katika tamko hilo wameeleza kuwa iwapo mgogoro wa DRC hautashughulikiwa mapema kunahatari ya kuwa mbaya zaidi na kuhatarisha amani ya kanda nzima. Kutokana na tishio hilo wadau wa asasi za kiraia wamesisitiza kuongezwa kwa juhudi katika kutatua mgogoro huo huku wakitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano hayo, kuondolewa kwa vikosi vya kigeni vilivyoingia DRC bila mwaliko na kupatikana kwa haki kwa waathirika wa vita hiyo. Vilevile wameunga mkono azimio la mkutano wa marais kuunganisha mchakato wa Rwanda na Nairobi ili kuwezesha mazungumzo kati ya DRC na Rwanda na kusisitiza umuhimu wa kusitisha mapigano.
1
3
28
Akizungumza na Vyombo vya Habari jana tarehe 08/02/2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa alisema watotohao wamepatikana wakiwa wamefichwa katika nyumba namba 8 iliyopo katika Mtaa wa Nyagoloboya Kata ya Nyegezi wakiwa pamoja na watekaji. Amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwanusuru Wanafunzi wawili (02) wa Shule ya Blessing Model School waliokuwa wametekwa Februari 05, 2025 wakiwa salama. Hata hivyo, amesema Askari wa Jeshi la Polisi walilazimika kutumia risasi za moto na kuwajeruhi watekaji baada ya kuonesha nia ya kutaka kuwashambulia maaskari wakiwa na silaha kama mapanga, rungu na jambia majeraha yaliyosababisha watekaji hao kupoteza maisha. Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kuokoa maisha ya watoto hao walioleta taharuki kubwa katika jamii.
0
0
5
Katika barua ya wazi kwa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), muungano wa makundi ya waasi na kisiasa nchini Congo la Alliance Fleuve Congo (AFC) unaojumuisha kundi la M23, umejitokeza kupinga vikali uamuzi wa SADC wa kupeleka vikosi vyake Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Katika barua hiyo iliyoandikwa saa chache kabla ya mkutano wa pamoja wa SADC na EAC, AFC inasisitiza kuwa mgogoro wa DRC ni wa kisiasa, wa utambulisho na wa ndani, hivyo unahitaji suluhisho la ndani badala ya maingilio ya kijeshi kutoka nje. Mratibu wa AFC, Corneille Nangaa Yobeluo, ameandika: "Tunachukua hatima ya nchi yetu mikononi mwetu kwa mujibu wa Katiba ya DRC. Hatuwezi kuruhusu vikosi vya nje kusaidia serikali isiyo halali ambayo inakandamiza watu wake na kuhatarisha umoja wa taifa." Katika barua hiyo, AFC inabainisha kuwa M23 ni sehemu ya harakati yao, wakisisitiza kuwa mapambano yao si uasi bali ni mapinduzi ya kikatiba dhidi ya kile wanachokiita "utawala wa mabavu wa Félix Tshisekedi." Wanaeleza kuwa utawala huo umegeuka kuwa tishio kwa wananchi kwa kujihusisha na ukandamizaji wa kisiasa, rushwa, na kuendeleza siasa za kikabila. AFC inashutumu vikali SADC kwa kutumia mkataba wa ulinzi wa pamoja (SADC Mutual Defence Pact, 2003) kama sababu ya kuingilia mgogoro huo. Wanasema kuwa mkataba huo unasisitiza kutohusisha majeshi ya nje katika masuala ya ndani ya nchi mwanachama isipokuwa tu pale ambapo kuna uvamizi wa nje. "Jeshi la SADC linajihusisha na vita vya ndani vya DRC kwa kuunga mkono utawala unaowakandamiza wananchi wake. Huu si ulinzi wa amani, bali ni kuchochea vita vya ndani." Anaonya Nangaa. Aidha, barua hiyo inamshutumu Rais wa DRC Felix Tshisekedi kwa kugeuza jeshi lake kuwa chombo cha ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa na kwa kushirikiana na vikundi vya wapiganaji wa kigeni kama FDLR, jambo ambalo AFC inadai kuwa ni tishio kwa wananchi wa DRC na ukanda mzima wa Maziwa Makuu.
4
4
75
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameendela kukanusha tuhuma za kuhusika kuchochea vita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku akieleza chanzo cha vita hiyo katika Mkutano wa pamoja wa EAC na SADC. Paul Kagame amesema: "Vita hii ilianzishwa na DRC na sio chochote kutoka Rwanda. Ililetwa tu na kuwekwa kwenye mabega yetu na kisha tukaambiwa tuimiliki. Hatuwezi kuimiliki vita hii na hakuna wa kutuuliza swali juu hilo" "DRC haiwezi tu kutuambia tunyamaze wakati wanaongeza tatizo la usalama dhidi ya nchi yetu. Hakuna anayeweza kutuambia tunyamaze" "Tumekuwa tukiiomba sana DRC na viongozi wake kwa muda mrefu, tumewashirikisha masuala yetu na kuwataka DRC wayashughulikie, lakini walikataa" Aliongeza kuwa "Hatuwezi kuendelea kukumbatua matatizo milele. Kinachotokea huko ni vita vya kikabila ambavyo vimezuka kwa muda mrefu, vikisababishwa na kunyima haki za watu na kisha kushambulia Rwanda" "Ni lazima kutambua haki za watu na kuchukua hatua na kutatua suala hilo" "Hebu tuutumie mkutano huu kwa namna ambayo itatilia maanani mambo haya yote kwa uzito, na kutafuta suluhu la kudumu" Rais Kagame katika Mkutano wa pamoja wa EAC-SADC.
2
1
22
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Ndele Jailos Mwaselela, ameendelea kutekeleza Ahadi zake kwa chama hicho ambapo Mwezi huu Februari 2025 amesema atakamilisha katika Wilaya ya Mbeya Vijijini. Amesema leo Februari 8,2025 atakabidhi bati Kata ya Isangala kama walivyoomba, kisha kuendelea na Kata zingine. Mara tu baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo Februari 14,2023 alifanya ziara katika Wilaya zote na kutekeleza Ahadi katika Wilaya ya Kyela, Rungwe, Chunya na Mbeya Vijijini. Katika Wilaya ya Kyela alitoa Mbao za kutosha jengo Zima kuezeka ofisi ya Wilaya hiyo, Rungwe alikarabati ofisi, Chunya alitoa Tofali ngazi ya Wilaya na Mbeya Vijijini pia alitoa Tofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wilaya ambako pia alipokea maombi ya ukarabati wa ofisi za Kata za Chama hicho. Katika maombi hayo, amesema atakamilisha Ahadi yake ya kukarabati ofisi za Chama hicho ndani ya Mwezi huu kutokana na uhitaji wa kila Kata. Mbeya Vijijini ina Kata za Serikali 28 huku chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa na Kata 32.
2
2
20
"Kinachotokea huko ni vita vya kikabila ambavyo vimezuka kwa muda mrefu, kunyima haki za watu na kisha kushambulia Rwanda, Ni lazima kutambua haki za watu na kuchukua hatua na kutatua suala hilo" Vita hii ilianzishwa na DRC na sio chochote kutoka Rwanda. Ililetwa tu na kuwekwa kwenye mabega yetu na tukaambiwa tuimiliki. Hatuwezi kuimiliki. Hakuna swali juu yake" "Hebu tuutumie mkutano huu kwa namna ambayo itatilia maanani mambo haya yote kwa uzito, na kutafuta suluhu la kudumu" Rais wa Rwanda.
3
2
41
"Inanipa furaha na heshima kubwa kuwakaribisha nyote katika Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, na hasa zaidi katika jiji la Dar es Salaam, mbingu ya amani. Kwa ajili ya Mkutano huu muhimu wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, ulioitishwa kujadili hali ya usalama iliyopo Mashariki mwa DRC. Tanzania ina heshima kubwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu wa ngazi ya juu, na inasalia na nia ya kudumu kwa lengo la kuhimiza amani na usalama ndani, kanda na kwingineko,” Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0
1
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Februari, 2025. Mkutano huo pamoja na mambo mengine unajadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
0
1
15
Rais Paul Kagame wa Rwanda akiwasili Ikulu, Dar es Salaam, kushiriki mkutano wa pamoja wa wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika leo Februri 08, 2025 kujadili hatima ya mgogoro nchini Congo. Ikumbukwe kuwa Paul Kagame, anatuhumiwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaopiga na majeshi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuchochea mgogoro huo.
0
5
49
VIDEO: Mkutano wa pamoja wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unafanyika Jijini Dar es Salaam, kujadili hatima ya mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mkutano huo unafanyika huku vikundi vya waasi chini ya Alliance Fleuve Congo (AFC/M23) vikiwa vimeshikilia miji ya Goma, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Nyabibwe vikielekea Bukavu.
3
9
78
Rais wa Jamhuri ya Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. William Samoei Ruto amewasili Nchini Tanzania na kupokelewa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso. Mhe. Rais Ruto amewasili kuhudhuria Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya za EAC na SADC utakaofanyika nchini tarehe 8 Februari, 2025. Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili namna ya kupata ufumbuzi kuhusu hali ya usalama Mashariki mwaJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
0
0
4
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Uhuru kilichopo Wilaya ya Urambo mkoani Tabora umekamilika. Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Februari 07 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Urambo, Mhe. Margaret Sitta aliyetaka kufahamu Serikali itakamilisha lini kituo hicho cha kupoza umeme na lini kitaanza kufanya kazi. "Mhe. Spika ujenzi wa kituo cha kupoza umeme umeshakamilika, hivi sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme, ikikamilika kituo hicho kitaanza kufanya kazi." Amesema Mhe. Kapinga Akijibu swali la Mbunge wa Nanyumbu, Mhe. Ally Mhata aliyetaka kufahamu lini Serikali itashusha bei ya kuunganisha umeme katika Kata za Mangaka na Kilimanihewa kama maombi yalivyowasilishwa Wizarani, Mhe. Kapinga amesema kutokana na hali halisi ilivyo nchini, kuna maeneo ya vijiji na Vijiji Miji ambapo maeneo ya vijiji yanaunganishwa na umeme kwa gharama ya shilingi 27,000. Ameongeza kuwa, maeneo yenye sura ya Vijiji-Miji yanaunganishwa kwa gharama ya shilingi 320,960 hivyo kwa maeneo ya Kata ya Mangaka na Kilimahewa yenye sura ya Vijiji Miji yana unganishwa umeme kwa gharama ya shilingi 320,960. Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuangalia kama kuna uwezekano wa kufanya maboresho ya gharama kutokana na tathmini iliyofanyika. Kuhusu Vitongoji 105 ambavyo havijapata umeme Wilaya ya Nanyumbu, Mhe. Kapinga amesema hivi sasa Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji ikiwemo Vitongoji 15 kwa Mbunge na kwa mwaka ujao wa fedha vitaongezwa Vitongoji vingine 38 ili kupunguza idadi ya vitongoji hivyo 105.
0
0
2
VIDEO: Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (The Mwalimu Nyerere Foundation) Joseph Butiku ameongoza kikao cha asasi za kiraia kutoka nchi kumi na mbili za Afrika kujadili mgogoro unaoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Kikao hicho kinafanyika kuanzia leo Februari 7 hadi kesho Februari 8 2025, kikiambatana na mkutano utakaofanyika Jijini Dar es Salaam mnamo Februari 8, 2025, ukiwakutanisha Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kujadili mzozo huo.
0
0
3
Waasi wa kundi la M23 wameanzisha mashambulizi mapya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni siku chache kabla ya marais wa Rwanda na Kongo kuhudhuria mkutano wa kujadili kusitisha mgogoro huo. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na viongozi wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Mapigano makali yalizuka alfajiri ya Jumatano karibu na Nyabibwe, takriban kilomita 100 (maili 60) kutoka Bukavu ambapo ni kilomita 70 kutoka uwanja wa ndege wa jimbo hilo. Awali, katika kutangaza usitishaji wa vita M23 walisema "hawana nia ya kuchukua udhibiti wa Mji wa Bukavu au maeneo mengine". Kwa upande mwingine msemaji wa serikali ya Kongo, Patrick Muyaya alisema "Hili ni thibitisho kwamba usitishaji vita wa upande mmoja ambao ulitangazwa na M23 kama kawaida, ni njama na uongo" Aliongeza kuwa "Kwa zaidi ya miaka mitatu ya mapigano kati ya kundi linaloungwa mkono na Rwanda (M23) na jeshi la Kongo, nusu ya matamko ya usitishaji mapigano na mapatano yaliyotangazwa, yalivunjwa bila utaratibu. Vyanzo vya ndani na kijeshi vilisema katika siku za hivi karibuni, pande zote zilikuwa zikiimarisha wanajeshi na zana katika eneo hilo.
0
0
10