![Anna Tibaijuka Profile](https://pbs.twimg.com/profile_images/1543729539/anna_tibaijuka_1_x96.jpg)
Anna Tibaijuka
@AnnaTibaijuka
Followers
35K
Following
33
Statuses
401
Retired 1. UN Under Secretary General & 2. Executive Director UNHABITAT 3. Tanzanian MP and Minister.
Dar-es-Salaam
Joined September 2011
The elephant in the room is whether the government of DRC based in Kishasa over 2500 km away from Eastern Congo is able to function effectively. Since independence the Kinshasa based government has never been effectively in control of the vast territory. The abundance of minerals and natural resources makes things worse. A true curse for the local people... given the greed by national regional and international actors. Africa must shed colonial hangover by clinging to outdated ideas. DRC needs a fully fledged federal government to function efficiently. A unitary state is not working well at all. What will it take for this reality to be recognised?
14
38
93
RT @benryanwriter: BREAKING: Secretary of State Marco Rubio provides waiver for @PEPFAR to provide HIV medications to poor nations. The Tr…
0
178
0
BREAKING NEWS KUTOKA KWA RAIS TRUMP INAYOTUHUSU NI AFYA ZA MAMILIONI YA WATU KUWA HATARINI. Ikiwa uamuzi wake kusitisha misaada kwa mashirika ya afya duniani hasa PEPFAR na GLOBAL FUND yatatekelezwa ni kiama. Upatikanaji wa madawa ya kuongeza kinga za mwili ARVs utaathirika. Ninashauri Wizara ya Afya kuufahamisha umma wa waTanzania je ni hatua gani za haraka zinachukuliwa kutathmini jambo hili na kuchukua hatua stahiki?. Ikibidi African Union waitishe kikao maalum kuangalia swala hili na kuweka mkakati wa pamoja. Waathirika wa gonjwa hili la UKIMWI ni waAfrika na ugonjwa haujulikani ulitoka wapi?. Tujitetee. Aidha juhudi za kuthibiti maambukizi ya virus vya ukimwi ziwekewe nguvu mpya. Upatikanaji wa ARVs utakuwa mgumu. Na kununua ARVs kibiashara ni jambo litakalohitaji bajeti kubwa na uwezo wa taifa kwa ujumla ni mdogo. Na jambo limekuwa la ghafla. Waathirika wengi hawana uwezo kununua madawa hayo wenyewe maisha yao yote. Afya zao zikidhoofika itatumika gharama kubwa kuwauguza hivo kusababisha umaskini na vifo. Pia bila ARVs maambukizi yatashika kasi mpya. Tuwe macho
438
383
2K
Naungana na wengine kuwapongezeni CHADEMA kukamilisha uchaguzi wenu kwa uwazi na ushindani wa hoja na kuibuka wamoja na imara zaidi. Kila mmoja wenu kaibuka mshindi wa kile alichokipigania hadi mwisho. Pongezi kubwa kwa wanachama wa majimboni tuliowashuhudia mki wakumbusha wajumbe wenu chaguo lenu ni lipi yaani kudai utaratibu wa PLEDGED DELEGATE kama ilivyo Marekani. Mfumo huo ukichukuliwa hofu za rushwa kwa wajumbe zitatoweka kabisa na kuimarisha demokrasia kwani mjumbe anaingia ukumbini kutangaza kura kwa mujibu wa maoni ya wanachama wake. Sio kujiamulia. Hiyo ndiyo demokratia ya kweli. Tuendelee kujifunza. Tutafika. Umoja na mshikamano kwenye picha ya waheshimiwa Lissu na Mbowe mkipongezana ni mfano wa kuigwa kote nchini. Tunajenga nyumba moja. Tusigombanie fito.
176
433
3K
MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM TAIFA 19-1-2025. Naungana na wengi kukupongezini kufanya maamuzi sahihi. Kuwateua Rais Samia na Rais Mwinyi kutetea nafasi zao katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025. Pia pongezi kumteua Katibu Mkuu wa CCM Balozi dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza Tz Bara. Uzoefu kutoka nchi za demokratia ya Uraisi mfano Marekani ni kwamba faida zake zinazidi hasara kwani unalinda umoja, utulivu na mshikamano wa chama, unamuwezesha Rais aliye madarakani kuendelea kufanya kazi yake bila wasiwasi, unalinda heshima na imani ya wapiga kura katika Rais aliye madarakani hivo kumpa nafasi nzuri kushinda uchaguzi mkuu. Hasara yake kubwa ni kuwanyima nafasi waliotaka kushindania nafasi hiyo lakini maslahi mapana ya chama ni muhimu zaidi ya maslahi ya mwanachama mmoja mmoja. KAZI IENDELEE.
15
14
116
Kama hii video siyo fake wazazi tafadhali tofautisheni shule na mahabusu za watoto kwa kisingizio cha ufaulu mzuri ambao hauna maana kama gharama yake ni mtoto aliyeathirika kisaikologia. Ndiyo maana shule zangu za wasichana BARBRO JOHANSON Ya Dsm na KAJUMULO ya Bukoba haziruhusu viboko. Tunalea kwa kauli na tuko vizuri. KARIBUNI. Simu 0686 18 96 05
55
30
140
RT @Mwabuk2Boniface: He is a servant of the living and true God, a mediator, a lover of justice, and one who is unashamed of the gospel of…
0
172
0
Jaji Werema alikerwa na mhe Kafulila kuwa kundi moja na Hayati mhe Nimrodi Mkono ambaye kwa upande wake aliona Jaji Werema mbaya kwa kufunga "shamba lake", yaani kusitisha mwendelezo wa kesi ya miaka mingi kati ya IPTL na Tanesco huko London ambapo Mkono alishalipwa zaidi ya shs Bilioni 62 za uwakili na TANESCO
0
0
4
Tamasha la pili la IJUKA OMUKA 2024 (KUMBUKA NYUMBANI) Bukoba. Limefanikiwa sana kuhamasisha maendeleo na utamaduni wa vyakula na mavazi asilia mwendelezo wa BUHAYA FESTIVAL iliyofanyika Oktoba Mlimani City DSM. Shukrani mgeni rasmi Mhe Dotto Biteko naibu Waziri Mkuu. Pongezi muandaaji RC wetu hodari Mhe Hajat Fatma Mwassa - Ma KATALEMWA (asiyechoka), Waziri Mambo ya Ndani Mhe Innocent Bashungwa. Kwa kauli moja wadau wote tumempongeza Mhe Rais Samia kumteua "Ma Katalemwa" kuinua mkoa kwa hamasa zake chanya kutupa moyo na matumaini mapya. "Tweyememu. TWAKILA".. KAZI IENDELEE. Vazi la wanawake miaka ya 50 liliitwa LIBATA EMPIYA (max dress) ndilo hilo. Tofauti na Rwanda Muhaya anajisitiri mabegani na mtandio wake.
57
61
516
THAMANI YA DOLA NA UHABA WAKE KUGEUKA GHAFLA NA IKAWA NI SHILINGI YA TANZANIA INAYOPANDA THAMANI. KULIKONI? Tatizo la kuyumbayumba kwa sarafu katika mfumo wa soko huria ni jambo lisiloepukika lakini si kwa kasi kubwa inayoendelea. Benki Kuu ina jukumu na mbinu za kuingilia kuthibiti hali hii kuepusha athari zake kiuchumi , kibiashara na kulinda ajira. Benki Kuu hukabiliana na tatizo kwa kuongeza upatikanaji wa sarafu inayopungua katika mabenki ya biashara ili kutunza uimara na utulivu wa sarafu yetu. Katika nchi inayoendelea kama Tanzania na inategemea biashara ya nje (exports) athari za thamani ya sarafu yake kupanda na kuwa na nguvu dhidi ya dola ni kupunguza ushindani wetu kuuza bidhaa nje kwani wanunuzi wataona ni aghari na kwenda kununua kwingineko. Mazao yetu ya kuuza nje yaweza kukosa masoko na bei za wakulima kushuka na pia watalii kupungua. Viwanda vyetu vyaweza kushindwa kushindana na bidhaa zitakazoingizwa kwa wingi kutoka nje hivo kuua uzalishaji wetu na ajira. Ukuaji wa uchumi utapungua kutokana na ukosefu wa mzunguko mzuri wa fedha. Mahala pa kuanzia ni kwa Benki kuu kupunguza riba ili kuongeza fedha katika mzunguko kwenye benki za biashara. Riba za tarakimu mbili hazijakaa sawa. Zinaathiri uchumi. Tumezizoea lakini si sawa.
174
136
752
SHIRIKA LA AFYA DUNIANI - WHO: UTARATIBU WA KUMPATA MKURUGENZI MPYA WA KANDA YA AFRIKA BAADA YA UMAUTI KUMKUTA MTEULE HAYATI DR NDUGULILE. Wengi mmenipigia simu kuulizia jambo hili. Ninaamini mchakato wa uchaguzi utaanza upya kwani WHO haina utaratibu wa kumteua aliyekuwa amemfuata Mteule kwa kura kushika nafasi hiyo. Aidha hakuna utaratibu kuhusu mbadala kutoka nchi yake ingawaje Executive Bodi ya WHO inaweza kuamua vinginevyo. Kinyang'anyiro kikirudiwa nina imani Tanzania itakuwa na haki nayo kuteua mgombea mwingine kuwania nafasi hiyo upya na ushindi unaweza kupatikana tena. Hakuna shaka Prof Janabi anatosha ila kila uchaguzi una siasa zake. Sympathy vote inaweza kutubeba au kutubwaga. Ni kusubiri tuone. Apumzike kwa amani Dr Ndugulile. Katuachia majonzi makubwa.
81
91
829
MiAKA 63 YA UHURU. TUJIPONGEZE. Kati ya Watanzania 68.5 milioni wa leo ni asilimia 2.6% tuliozaliwa kabla ya Uhuru 09.12.1961. Ninamshukuru Mungu kuwa miongoni mwao. Tumepiga hatua kubwa kimaendeleo kwa sababu ya kudumisha amani kwa Siasa safi na uongozi bora. Tuwe makini tusipoteze tunu hizi tusijeharibikiwa kama wenzetu wengi. Kuheshimiana tunapotofautiana. Kupeana mawazo bila uhasama na kejeli. Ndizo ishara za taifa lenye miaka 63 ya uhuru. Taifa linaloenzi waasisi wake waliosimika misingi na siri ya mafanikio yetu.
39
28
138
28.03.1960. St. Peters Basilica. Vatican City. Laurean Rugambwa was created the 1st Native African Cardinal of the Catholic Church by Pope John XXIII. Today we commemorate his 27th year memoriam ( 12.07.1912 - 08.12.1997). May this iconic son of Africa RIP. His legacy endures. Notable was pioneering quality education for girls at Rugambwa high school in Bukoba where I studied under his sponsorship.
8
62
261
Ta Kardinali Laurean Rugambwa. 12.07.1912 - 08.12.1997. Mlezi wetu. Bila maono upendo na ubunifu wako wasichana tuliosoma shule yako ya sekondari Rugambwa ndoto zetu zisingetimia. Tunakushukuru na kuamini raha ya milele umejaliwa kwa maisha yako ya kujitoa kitakatifu. RIP. Baada ya miaka 27 bado nuru yako inatuangaza. Ni wajibu wetu tuliobahatika kukufahamu kutoa ushuhuda kwa Baba Mtakatifu impendeze kukutambua kama Mwenyeheri na Mtakatifu. Ee Mungu twakuomba sisi wanao.
34
67
776
POLENI WAHANGA WA GHOROFA lililoanguka ila Ujenzi wa maorofa Kariakoo. NI JANGA KAMA LA JANGWANI. Kwa sheria za mipango miji ilitakiwa viwanja 4 vya high density viunganishwe mbele na nyuma kipatikane kiwanja kimoja kikubwa cha kujenga orofa imara yenye basement kubwa kupaki magari. Orofa inayofunguka kwenye mtaa wa mbele na nyuma. Awali katika awamu ya Tatu Ushauri huo wa watalaamu wa mipango miji ulishapuuzwa na viongozi kwa presha ya wawekezaji kwa hiyo maorofa Kariakoo na kwingineko yanajengwa kiholela kwenye viwanja visivyokidhi vigezo. Pamoja na madhaifu ya usimamizi wa UJENZI KIUHANDISI Ni vigumu majengo kuwa imara bila kuwa na eneo la kutosha kujenga kitako yaani base foundation stahiki. Naendelea kuhimiza kurekebisha kosa hilo. Sasa tunavuna hasara kubwa ya upotevu wa mali.. na maisha na fursa za ajira na aibu ya kushindwa kusimamia viwango vya ujenzi Miaka 63 baada ya uhuru.. Tuwaombee wahanga auheni na waliopoteza maisha pumziko la milele. Naendelea kushauri viwango vya vertical development vizingatiwe kuanzia sasa. Tujisahihishe.
247
537
2K